Yesu Alisha Watu Elfu Tano
1Baadaye, Yesu alivuka hadi ng’ambo ya pili ya ziwa la Gali laya, ambalo pia huitwa bahari ya Tiberia. 2Watu wengi walikuwa wakimfuata kwa sababu walikuwa wamemwona akiponya wagonjwa kwa njia za ajabu. 3Yesu alikwenda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia.
5Yesu alipotazama aliona umati mkubwa wa watu wanamfuata. Akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ya kuwalisha watu hawa?” 6Alisema hivi kumjaribu Filipo maana yeye mwenyewe ali jua atakalofanya.
7Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapatia watu hawa japo kila mtu apate kipande kidogo.”
8Mmoja wa wanafunzi wake, aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema, 9“Kuna mvulana mmoja ana mikate mitano na samaki wawili. Lakini hivi vitafaa nini kwa umati wote huu?”
10Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Zilikuwapo nyasi nyingi mahali hapo, kwa hiyo watu wapatao elfu tano wal iweza kukaa chini. 11Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia wale watu waliokuwa wamekaa. Akawagawia pia na hao samaki wawili, kila mtu kiasi alichotaka. 12Watu wote wali pokwisha kula kiasi cha kutosha, aliwaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vipande vilivyobaki, kisipotee kipande cho chote.” 13Basi wakakusanya vipande vya ile mikate mitano, wakajaza vikapu kumi na viwili.
14Watu walipoona muujiza huu alioufanya Yesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii tuliyekuwa tukimtazamia!”
15Yesu, akijua kwamba walitaka kumlazimisha awe mfalme wao, aliondoka hapo, akaenda milimani peke yake.
Yesu Atembea Juu Ya Maji
16Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kuelekea ziwani. 17Wakaingia katika mashua, wakaanza kuvuka kwenda Kap ernaumu. Wakati huo giza lilikuwa limeanza kuingia na Yesu ali kuwa hajatokea bado.
18Wakati huo upepo mkali ulikuwa unavuma na bahari ikaanza kuchafuka. 19Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo upatao kar ibu kilometa nane, walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikari bia mashua! Wakaogopa sana. 20Lakini Yesu akawaambia, “ Ni mimi; msiogope.” 21Ndipo wakafurahi, wakamkaribisha kwenye mashua, na mara wakafika walipokuwa wanakwenda.
Watu Wanamtafuta Yesu
22Kesho yake, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo ya pili waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila waliondoka peke yao. 23Lakini mashua nyingine kutoka Tiberia zilikuwa karibu zina fika mahali pale walipokula mikate baada ya Yesu kumshukuru Mungu. 24Basi wale watu walipotambua kwamba Yesu hayupo hapo, wala wanafunzi wake hawapo, waliingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu kumtafuta.
Yesu Ni Mkate Wa Uzima
25Walipomkuta Yesu ng’ambo ya ziwa wakamwuliza, “Rabi, umefika lini huku?” 26Yesu akawajibu, “Ni wazi kwamba ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza ninayofanya, isipo kuwa mnanitafuta kwa sababu mlikula mikate mkashiba. 27Msishug hulikie sana chakula kiharibikacho bali shughulikieni chakula kidumucho; chakula cha uzima wa milele. Chakula hicho, nitawapeni mimi Mwana wa Adamu, ambaye Baba Mungu mwenyewe amenithibit isha.”
28Wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuonekane kuwa tunatenda kazi ya Mungu?” 29Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii: mumwamini yeye aliyenituma.” 30Wakamwambia, “Utafanya ishara gani ya muujiza, tuone ili tukuamini? Utafanya jambo gani? 31Baba zetu walikula mana jangwani. Kama Maandiko yanavyosema, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni wakala.”’
32Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni. Baba yangu ndiye anayewapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33Kwa maana mkate wa Mungu ni yule aliyeshuka kutoka mbinguni na ambaye anatoa uzima kwa ulimwengu.”
34Wakamwambia, “Bwana, tupatie mkate huo sasa na siku zote.
35Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe. 36Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki kuamini. 37Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”
41Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42Wakasema, “Huyu si Yesu mwana wa Yusufu? Na baba yake na mama yake si tunawajua? Anawezaje basi kutuambia kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
43Lakini Yesu akawaambia, “Acheni kunung’unika. 44Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama Baba aliyenituma hakumvuta kwangu; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45Kama manabii walivyoandika, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Ye yote amsikilizaye Baba na kuji funza kutoka kwake, huja kwangu. 46Hii haina maana kwamba kuna mtu aliyekwisha kumwona Baba. Ni yule aliyetoka kwa Mungu peke yake, ndiye aliyekwisha kumwona Baba. 47Nawaambieni kweli: anayeamini anao uzima wa milele. 48Mimi ni mkate wa uzima. 49Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”
52Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”
53Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sina gogi huko Kapernaumu.
Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu
60Wengi wa wanafunzi wake waliosikia maneno haya walisema, “Mafundisho haya ni magumu! Ni nani awezaye kukubaliana nayo?”
61Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walikuwa wakilalamika kuhusu mafundisho yake. Kwa hiyo akawauliza, “Mafundisho haya yanawaudhi? 62Ingekuwaje basi, kama mngeniona mimi Mwana wa Adamu nikirudi mbinguni nilikotoka? 63Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima. 64Lakini baadhi yenu hamuamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini na yule ambaye angemsaliti. 65Akaendelea kusema, “Ndio sababu nili waambia kwamba hakuna awezaye kuja kwangu kama Baba hakumwe zesha.”
66Tangu wakati huo wanafunzi wake wengi waliondoka wakaacha kumfuata. 67Yesu akawauliza wale wanafunzi kumi na wawili, “Ninyi pia mnataka kuondoka?” 68Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu.”
Mungu.”
70Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni shetani!” 71Hapa alikuwa anamsema Yuda, mwana wa Simoni Iskariote ambaye, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, baadaye angemsaliti Yesu.