Yesu Ahudhuria Sikukuu Ya Vibanda Yerusalemu
1Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Aliamua kutokwenda Yudea kwa sababu Wayahudi huko wali taka kumwua. 2Sikukuu ya Vibanda ilipokaribia, 3ndugu zake Yesu walimwambia, “Ni vema utoke hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wapate kuona miujiza unayofanya. 4Mtu anayetaka kujulikana, hafanyi mambo yake kwa siri. Kwa kuwa unafanya mambo haya, jion yeshe kwa ulimwengu.” 5Hata ndugu zake hawakumwamini.
6Yesu akawajibu, “Wakati wangu wa kwenda huko haujafika. Ninyi mnaweza kwenda wakati wo wote. 7Ulimwengu hauwachukii ninyi lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. 8Ninyi nendeni kwenye sikukuu, lakini mimi sitahudhuria sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” 9Baada ya kusema hivyo, akabaki Galilaya. 10Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye sikukuu, yeye pia alikwenda kwa siri. 11Huko kwenye sikukuu viongozi wa Wayahudi walikuwa wakimtafuta na kuulizana, “Yuko wapi?”
12Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Yesu. Baadhi ya watu walisema, “Ni mtu mwema” na wengine wakasema, “Sio, ana wadanganya watu.” 13Lakini hakuna aliyemsema wazi wazi maana wote waliwaogopa viongozi wa Wayahudi.
Yesu Atangaza Mamlaka Yake
14Katikati ya sikukuu, Yesu alikwenda Hekaluni akaanza kuwafundisha watu. 15Viongozi wa Wayahudi walistaajabia mafund isho yake wakasema, “Amefahamuje mambo haya naye hakusoma?”
16Yesu akawajibu , “Mafundisho yangu hayatoki kwangu. Yanatoka kwake yeye aliyenituma. 17Mtu ye yote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa mamlaka yangu mwenyewe. 18Mtu anayesema kwa mamlaka yake mwenyewe hufanya hivyo kwa kutaka kujitukuza. Lakini mtu anayetafuta kumtukuza Mungu aliyemtuma, ni mwaminifu na hana udhalimu wo wote. 19Kwani Musa hakuwapeni sheria? Mbona hakuna hata mmoja wenu anayetii sheria? Kwa nini mnataka kuniua?”
21Yesu akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkas taajabu. 22Lakini kwa kuwa Musa aliwaamuru kutahiri watoto wenu wa kiume, ingawa kwa kweli si Musa aliyeanzisha desturi hii ila ni mababu zenu, mnamtahiri mtoto hata siku ya sabato. 23Ikiwa mtu aweza kutahiriwa siku ya sabato kusudi sheria ya Musa isi vunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24Msitoe hukumu kwa kuangalia mambo juu juu. Hukumuni kwa haki.”
25Baadhi ya wakazi wa Yerusalemu wakasemezana, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumwua? 26Mbona anazungumza hadhar ani na wala hawasemi lo lote? Je, inawezekana wanafahamu kwa kweli kama yeye ndiye Kristo? 27Lakini huyu mtu tunafahamu ana kotoka, nasi tunajua ya kuwa Kristo atakapokuja hakuna atakayefa hamu atokako.”
28Yesu, akiendelea kufundisha Hekaluni, akatangaza kwa sauti, “Hivi kweli mnanifahamu na kufahamu ninakotoka? Mimi sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe. Yeye aliyenituma ni wa kweli na wala ninyi hamumjui. 29Lakini mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, na ndiye aliyenituma.”
30Basi viongozi wa Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumshika kwa sababu wakati wake ulikuwa bado haujatimia.
31Watu wengi kati ya wale waliokuwepo, walimwamini, wakasema, “Hivi Kristo akija, atafanya miujiza mikuu zaidi kuliko aliyoifanya huyu?”
Walinzi Wanatumwa Kumkamata Yesu
32Mafarisayo waliposikia minong’ono hii, wao pamoja na makuhani wakuu, waliwatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata.
33Yesu akasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitarudi kwake aliyenituma. 34Mtanitafuta lakini hamtaniona kwa kuwa huko nitakapokuwa, ninyi hamwezi kufika.” 35Basi viongozi wa Wayahudi wakaulizana, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambapo hatuwezi kumpata? Au anataka kwenda katika miji ya Wagiriki ambapo baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wagiriki 36Ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona, na huko nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika ?”’
Vijito Vya Maji Yaletayo Uzima
37Siku ya mwisho ya sikukuu, ambayo kwa kawaida ndio ili kuwa kilele cha sherehe, Yesu alisimama akasema kwa sauti kuu, “Mtu ye yote mwenye kiu na aje kwangu anywe. 38Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.” 39Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa.
40Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu walisema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.” 41Wengine wakasema, “Huyu ni Masihi!” Lakini wengine wakauliza, “Kwani Masihi kwao ni Gali laya? 42Je, Maandiko hayakusema kuwa Masihi atakuwa mzao wa Daudi na kwamba atazaliwa Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” 43Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati ya watu kumhusu Yesu. 44Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.
Kutokuamini Kwa Viongozi Wa Wayahudi
45Hatimaye wale walinzi wa Hekalu waliokuwa wametumwa kum kamata Yesu, walirudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo. Wakauli zwa, “Mbona hamkumleta ?”
46Wale walinzi wakajibu, “Hakuna mtu ambaye amewahi kufundisha kama yeye.” 47Mafarisayo wakajibu, “Ameweza kuwa danganya hata ninyi? 48Je, mmewahi kuona kiongozi ye yote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? 49Lakini huu umati wa watu wasiojua sheria ya Musa, wamelaaniwa.”
50Ndipo Nikodemo, yule aliyemwendea Yesu siku moja, ambaye alikuwa kati yao akauliza, 51“Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”
52Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza Maandiko nawe utaona kwamba hakuna nabii anayetokea Galilaya!” [ 53Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.