Nikodemo Amwendea Yesu Usiku
1Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo, 2alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
3Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
4Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”
5Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili. 8Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” 9Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli na huyaelewi mambo haya? 11Ninakwambia kweli, sisi tunazungumza lile tunalo lijua na tunawashuhudia lile tuliloliona, lakini hamtaki kutu amini! 12Ikiwa hamuniamini ninapowaambia mambo ya duniani, mtaniaminije nitakapowaambia habari za mbinguni? 13Hakuna mtu ye yote ambaye amewahi kwenda juu mbinguni isipokuwa mimi Mwana wa Adamu niliyeshuka kutoka mbinguni. 14Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu 15ili kila mtu aniaminiye awe na uzima wa milele . 16“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu. 18Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19Na hukumu yenyewe ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20Kwa kuwa kila mtu atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21Lakini kila mtu anayeishi maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo yake yanatokana na utii kwa Mungu.”
Yesu Na Yohana Mbatizaji
22Baadaye, Yesu alikwenda katika jimbo la Yudea pamoja na wanafunzi wake akakaa nao kwa muda na pia akabatiza watu. 23Yohana naye alikuwa akibatiza watu huko Ainoni karibu na Sal imu kwa sababu huko kulikuwa na maji mengi. Watu walikuwa wakim fuata huko naye akawabatiza. 24Wakati huo Yohana alikuwa bado hajafungwa gerezani.
25Ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kadhaa wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu swala la kutawadha. 26Basi wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe nga’mbo ya pili ya mto wa Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27Yohana akawa jibu, “Mtu hawezi kuwa na kitu kama hakupewa na Mungu. 28Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema mimi si Kristo ila nimetumwa nimtangulie. 29Bibi harusi ni wa bwana harusi. Lakini rafiki yake bwana harusi anayesimama karibu na kusikiliza, hufu rahi aisikiapo sauti ya bwana harusi. Sasa furaha yangu imekamil ika. 30Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi niwe mdogo zaidi.”
Aliyetoka Mbinguni
31“Yeye aliyekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. Anayetoka duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya hapa duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya watu wote. 32Anayashuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia lakini hakuna anayekubali maneno yake. 33Lakini ye yote anayekubali maneno yake, anathibitisha kwamba aliyosema Mungu ni kweli. 34Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu kwa maana Mungu amempa Roho wake pasipo kipimo. 35Baba anampenda Mwanae na amempa mam laka juu ya vitu vyote. 36Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”