Kifo Cha Lazaro
1Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika kijiji cha Bethania pamoja na dada zake wawili, Mariamu na Martha. 2Huyu Mariamu ndiye aliyempaka Bwana Yesu manukato miguuni na kumpangusa kwa nywele zake. 3Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” 4Lakini Yesu alipopata habari hizi alisema, “Ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea ili kudhihirisha utu kufu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi Mwana wa Mungu, nitatukuzwa. ”
5Kwa hiyo ijapokuwa Yesu aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro, 6alipopata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukaa huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. 7Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea.” 8Wanafunzi wake wakam wambia, “Mwalimu, utakwendaje tena Yudea ambako siku chache tu zilizopita Wayahudi walitaka kukupiga mawe?” 9Yesu akawajibu, “Si kuna masaa kumi na mawili ya mchana katika siku moja? Mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa maana kuna mwanga wa ulim wengu. 10Lakini mtu akitembea usiku hujikwaa kwa sababu hana mwanga nafsini mwake.”
11Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”
2Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.” 13Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi. 14Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa. 15Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla Lazaro kufa. Hii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni.” 16Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe pamoja naye.”
Yesu Ni Ufufuo Na Uzima
17Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita. 18Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu, 19Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. 20Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani. 21Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa. 22Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.” 23Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.” 24Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 25Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; 26na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?” 27Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.”
Yesu Analia
28Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita.” 29Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu. 30Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye. 31Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata. 32Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.” 33Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” 35Yesu akalia. 36Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!” 37Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”
Yesu Amfufua Lazaro
38Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. 39Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. 42Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.” 43Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!” 44Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”
Mpango Wa Kumwua Yesu
45Wayahudi wengi waliokuja kumfariji Mariamu, walipoona yaliyotokea wakamwamini Yesu. 46Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya. 47Kwa hiyo maku hani wakuu na Mafarisayo wakafanya baraza wakaulizana, “Tufa nyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48Kama tukimruhusu aendelee hivi, kila mtu atamwamini; na Warumi watakuja kuharibu Hekalu letu na taifa letu.” 49Lakini mmoja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu kwa mwaka ule akawaambia wen zake, “Ninyi hamjui kitu! 50Hamwoni kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, badala ya taifa lote kuangamia?” 51Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka ule, alikuwa anatabiri kuwa Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi; 52na pia kwa ajili ya watoto wa Mungu wal iotawanyika ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53Tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu. 54Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani, bali alitoka Bethania akaenda mikoani karibu na jangwa, kwenye kijiji kimoja kiitwacho Efraimu. Alikaa huko na wanafunzi wake.
55Wakati Pasaka ya Wayahudi ilipokaribia, watu wengi wali toka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajita kase kabla ya sikukuu. 56Watu walikuwa wakimtafuta Yesu, wakawa wanaulizana wakati wamesimama Hekaluni, “Mnaonaje? Mnadhani ata kuja kwenye sikukuu?” 57Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa kama yupo mtu anayefahamu alipo awafahamisha, ili wapate kumkamata.