Kaburi Tupu
1Jumapili asubuhi na mapema, kukiwa bado giza, Mariamu Mag dalena alifika kaburini akakuta lile jiwe lililokuwa limeziba mlango wa kaburi limeondolewa. 2Kwa hiyo akaenda mbio kwa Simoni Petro na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akawaambia, “Wameu chukua mwili wa Bwana kutoka mle kaburini na hatujui wameuweka wapi!” 3Petro na yule mwanafunzi wakaondoka mara kuelekea kabu rini. 4Wote wawili walikuwa wanakimbia lakini yule mwanafunzi akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akawahi kufika kaburini. 5Alipofika akainama na kuchungulia mle kaburini akaona ile sanda, lakini hakuingia ndani. 6Ndipo Petro akaja akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona ile sanda 7na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu kimekunjwa na kuwekwa kando ya ile sanda. 8Kisha yule mwanafunzi aliyewahi kufika kaburini naye akaingia ndani; akaona, akaamini. 9Kwa maana mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale Maandiko yaliyotabiri kuwa angefufuka kutoka kwa wafu. 10Wale wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.
Yesu Anamtokea Mariamu
11Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia akainama kutazama mle kaburini. 12Akaona malaika wawili wamevaa nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande wa miguuni na mwingine upande wa kichwani! 13Wakamwuliza Mariamu, “Mama, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui wamemweka wapi.” 14Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”
Yesu Anawatokea Wanafunzi Wake
19Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana! 21Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” 22Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”
Yesu Anamtokea Tomaso
24Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”
26Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.” 27Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.” 28Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”
30Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31Lakini hizi zimeandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.