Yohana 10

Mchungaji Mwema

1“Ninawaambia hakika, mtu asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya ndani kwa kupitia njia nyin gine, ni mwizi na mnyang’anyi. 2Anayepitia mlangoni ndiye mchun gaji wa kondoo. 3Mlinzi humfungulia mlango na kondoo hutambua sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza nje ya zizi. 4Akiisha watoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaifahamu sauti yake. 5Kondoo hawam fuati mtu wasiyemfahamu bali humkimbia, kwa sababu hawatambui sauti ya mgeni.” 6Yesu alitumia mfano huu lakini wao hawakuel ewa maana yake.

7Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. 8Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili. 11Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.

14Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”

19Maneno haya yalisababisha mafarakano tena kati ya Way ahudi. 20Wengi wao walisema, “Huyu amepagawa na shetani, kwa nini tuendelee kumsikiliza?” 21Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na shetani. Je, shetani anaweza kumpo nya kipofu?”

Yesu Anajitambulisha

22Ilikuwa sikukuu ya Utakaso wa Hekalu wakati wa majira ya baridi, 23na Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30Mimi na Baba yangu tu mmoja.”

31Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”

Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”

34Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”

39Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.

40Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42Na wengi wakamwamini Yesu.