Yesu Akamatwa
1Baada ya sala hii Yesu aliondoka na wanafunzi wake waka vuka kijito cha Kidroni wakaingia katika bustani iliyokuwa upande wa pili. 2Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. 3Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. 4Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia, “Ni mimi.” Yuda ambaye alimsaliti alikuwa amesimama na wale askari. 6Yesu alipowaambia, ‘Ni mimi,’ walirudi nyuma wakaanguka chini! 7Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakajibu, “Yesu wa Nazareti .” 8Yesu akawaambia, “Nimekwisha waeleza kuwa ni mimi; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi waachilieni hawa wengine waende.” 9Alisema haya ili lile neno alilosema lipate kutimia, ‘Kati ya wale ulionipa sikupoteza hata mmoja.’ 10Ndipo Simoni Petro akachomoa upanga aliokuwa amechukua akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo lilikuwa Malko. 11Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?” 12Kwa hiyo mkuu wa kikosi na askari wake pamoja na wale walinzi wa Hekalu waliot umwa na viongozi wa Wayahudi, wakamkamata Yesu wakamfunga mikono. 13Kisha wakampeleka kwanza kwa Anasi mkwewe Kayafa ambaye ali kuwa ndiye kuhani mkuu mwaka ule. 14Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri viongozi wengine wa Kiyahudi kwamba ingekuwa afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Petro Anamkana Yesu
15Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu kwa hiyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 16Lakini Petro alisimama nje karibu na mlango. Ndipo yule mwanafunzi mwin gine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda mlangoni, akamru husu amwingize Petro ndani. 17Yule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro aka jibu, “Hata! Mimi sio.” 18Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa mkaa ambao walikuwa wamewasha kwa sababu pale ukumbini palikuwa na baridi kali. Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
Kuhani Mkuu Amhoji Yesu
19Kuhani mkuu akamwuliza Yesu maswali kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. 20Yesu akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza wazi wazi mbele ya watu wote. Nimefundisha katika masinagogi na Hekaluni ambapo Wayahudi wote hukusanyika. Sijasema jambo lo lote kwa siri. 21Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize walionisiki liza nimewaambia nini. Wao wanajua niliyosema.” 22Mmoja wa wale walinzi akampiga Yesu kofi, kisha akasema, “Unathubutuje kumjibu kuhani mkuu hivyo?” 23Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo baya waeleze watu wote hapa ubaya niliosema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” 24Ndipo Anasi akampeleka Yesu kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa.
Petro Amkana Yesu Tena
25Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamwuliza, “Wewe ni mmoja wa wana funzi wake?” Petro akakana, akasema, “Mimi sio.” 26Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alim kata sikio, akamwuliza, “Je, sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 27Kwa mara nyingine tena Petro akakataa kwamba alimfa hamu Yesu. Wakati huo huo jogoo akawika.
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
28Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa wakampeleka kwenye ikulu ya gavana wa Kirumi. Ilikuwa ni alfa jiri. Wayahudi waliokuwa wanamshtaki Yesu hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa wachafu kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika sikukuu ya Pasaka. 29Kwa hiyo Pilato akatoka nje kuwaona akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” 30Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa ametenda maovu tusingemleta kwako.” 31Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote.” 32Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu atakavy okufa, yapate kutimia. 33Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akam wita Yesu akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” 34Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwe nyewe au kutokana na ulivyoambiwa kunihusu mimi?” 35Pilato akamjibu, “Unadhani mimi ni Myahudi? Watu wa taifa lako na maku hani wao wakuu wamekushtaki kwangu. Umefanya kosa gani?” 36Ndipo Yesu akamwambia, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Ingekuwa hivyo, watumishi wangu wangenipigania na kuhakikisha kuwa siwekwi mikononi mwa Wayahudi; lakini Ufalme wangu hautoki ulimwenguni.” 37Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema mimi ni mfalme. Nimezaliwa na nime kuja ulimwenguni kwa makusudi ya kushuhudia kweli. Mtu ye yote anayepokea yaliyo ya kweli anakubaliana na mafundisho yangu.” 38Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote ali lotenda mtu huyu.
39Lakini kuna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachilie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mngependa nimwachilie huru huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?” ’ 40Wao wakapiga kelele wakisema, “Hapana, usimwachilie huyo. Tufungulie Bar aba!” Baraba alikuwa mnyang’anyi.