Yohana 4

Yesu Na Mwanamke Msamaria

1Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kuba tiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana. 2Lakini kwa hakika Yesu hakubatiza, wanafunzi wake ndio waliokuwa wakibatiza watu. 3Bwana alipopata habari hizi aliondoka Yudea akarudi Galilaya. 4Katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.

5Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu. 6Kisima cha Yakobo kilikuwa hapo na kwa kuwa Yesu alikuwa amechoka kutokana na safari, aliketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

7Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.” 8Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula. 9Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria. 10Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”

11Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi? 12Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

13Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 14Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”

15Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuchota maji!”

16Yesu akamjibu, “Nenda kamwite mumeo, kisha uje naye hapa.” 17Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwam bia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!”

19Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu lakini ninyi Way ahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

21Yesu akamjibu, “Mama, niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwab udu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23Lakini wakati unakuja, tena umekwisha timia, ambapo wale wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii ndio anaowataka Baba. 24Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

26Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masihi.”

Masihi.”

27Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kum wona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” au “Kwa nini unazungumza naye?”

28Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaam bia watu, 29“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote nili yowahi kufanya! Je, yawezekana huyu ndiye Masihi?”

30Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.

31Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.”

32Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

33Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 34Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma, na kuikamilisha kazi yake. 35Si mnao msemo kwamba, ‘Bado miezi minne tutavuna’? Hebu yaangalieni mashamba, jinsi mazao yalivyoiva tayari kuvunwa! 36Mvunaji hupokea ujira wake, naye hukusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo aliyepanda mbegu na anayevuna, wata furahi pamoja. 37Ule msemo wa zamani kwamba , ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi hiyo; ninyi mmefaidika kutokana na jasho lao!”

39Wasamaria wengi walimwamini kutokana na ushuhuda wa yule mama alipowaambia kwamba, “Ameniambia mambo yote niliyowahi kutenda.” 40Kwa hiyo wale Wasamaria walipokuja, walimsihi akae kwao, naye akakaa kwa siku mbili. 41Watu wengi zaidi wakamwa mini kutokana na ujumbe wake. 42Wakamwambia yule mama, sasa hatuamini tu kwa sababu ya yale uliyotuambia bali kwa kuwa tumem sikia sisi wenyewe, na tunajua hakika kwamba yeye ni Mwokozi wa ulimwengu.”

Yesu Amponya Mtoto Wa Afisa

43Zile siku mbili zilipokwisha, Yesu aliondoka kwenda Gali laya. 44Yesu mwenyewe alikwisha sema kwamba nabii haheshimiki nchini kwake. 45Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.

46Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.

48Yesu akamwambia, “Ninyi watu hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza?”

49Yule afisa akajibu, “Bwana, tafadhali njoo kabla mwa nangu hajafa.” 50Yesu akamwambia, “Nenda nyumbani, mwanao ataishi.” Yule afisa akaamini maneno ya Yesu, akaondoka kurudi nyumbani. 51Alipokuwa bado yuko njiani, alikutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanae alikuwa mzima. 52Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53Yule baba akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao ataishi.” Kwa hiyo yeye, pamoja na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.

54Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.