1“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkapoteza imani yenu. 2Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu. 3Watu watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi. 4Lakini nimew aambia mambo haya kusudi muda huo utakapofika mkumbuke kuwa nili kuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
Kazi Ya Roho Mtakatifu
5“Lakini sasa ninakwenda kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ 6Kwa kuwa nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 7Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. 8Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 9Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12“Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia lakini hamwezi kuy apokea sasa. 13Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. 15Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.
Huzuni Na Furaha
16“Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 17Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”
19Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.
Ushindi
25“Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.” 29Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” 31Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami. 33Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”