Matendo Ya Mitume 9

Kuokoka Kwa Sauli

1Wakati huu wote Sauli alikuwa bado anaendelea na vitisho vyake vya kuwaangamiza kabisa wanafunzi wa Bwana. Akaenda kwa Kuhani Mkuu, akamwomba ampe barua ya kumtambulisha kwa masina gogi ya huko Dameski, ili akiwapata wafuasi wa ile ‘Njia Basi katika safari yake, alipokuwa akikaribia Dameski, ghafla nuru kutoka mbinguni iliangaza kumzunguka! Akaanguka chini! Na aka sikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” Sauli akajibu, “Ni nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikasema, “Mimi ni Yesu ambaye unamtesa. Lakini sasa inuka uingie mjini nawe utaambiwa la kufanya.” Wale waliokuwa wakisafiri na Sauli wakasimama kwa mshangao, wala hawakuweza kusema neno kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. Sauli akainuka na alipojaribu kufungua macho, hakuweza kuona kitu. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. Na kwa muda wa siku tatu akawa haoni kabisa, na hakula kitu wala kunywa cho chote.

10 Huko Dameski alikuwepo mfuasi mmoja jina lake Anania. Bwana akamwita Anania katika ndoto, “Anania! ” Akaitika, “Nipo hapa Bwana.” 11 Bwana akamwambia, “Amka uende barabara iitwayo Nyofu ukaulizie katika nyumba ya Yuda kuhusu mtu aitwaye Sauli wa Tarso. Yeye hivi sasa anaomba, na katika maono anamwona mtu 12 aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.” 13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi mambo ya kutisha ambayo mtu huyu anawatendea wataka tifu wako huko Yerusalemu. 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na kibali kutoka kwa Kuhani Mkuu awakamate wote wanaotaja jina lako.” 15 Lakini Bwana akamwambia Anania, “Nenda, kwa maana nimemchagua awe mtumishi wangu wa kulitangaza jina langu kwa mataifa na wafalme na kwa wana wa Israeli; 16 nami nitamwonyesha atakavyoteseka sana kwa ajili ya jina langu .” 17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Kisha akala chak ula, akapata nguvu tena. Alikaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski na 20 bila kukawia akaenda katika sinagogi akawash uhudia watu kwamba, “Yesu ni Mwana wa Mungu.”

Sauli Ahubiri Dameski

21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa wakasema, “Huyu si yule mtu aliyekuwa akiwatesa watu waliotaja jina la Yesu huko Yerusalemu, na ambaye amekuja hapa kwa shabaha ya kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wamefungwa kwa makuhani wakuu?” 22 Lakini Sauli alizidi kuhubiri kwa nguvu zaidi akathibitisha kabisa kwamba Yesu ndiye Kristo; hata Wayahudi walioishi Dameski hawa kuwa na lo lote la kupinga. 23 Baada ya siku nyingi kupita, Way ahudi walifanya mpango wa kumwua Sauli. 24 Lakini Sauli akapata habari za mpango huo. Wayahudi walikuwa wakilinda milango yote ya kutokea mjini, mchana na usiku ili akitoka wamwue. 25 Lakini wanafunzi wake wakamtoa nje ya mji usiku kwa kumpitisha mahali palipokuwa na nafasi katika ukuta wa mji, akiwa ndani ya kapu kubwa.

Sauli Atoa Ushuhuda Wake Yerusalemu

26 Sauli alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na waamini lakini wao walimwogopa kwa maana hawakuamini ya kuwa kweli ali kuwa amemwamini Yesu. 27 Lakini Barnaba akamchukua Sauli akampeleka kwa wale mitume akawaeleza jinsi Sauli alivyokutana na Yesu njiani akienda Dameski na Yesu akasema naye. Pia akawaeleza jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Kwa hiyo Sauli akakaa nao akishirikiana nao na aki hubiri wazi wazi kwa jina la Yesu kila mahali huko Yerusalemu.

29 Lakini alipowahubiria Wayahudi wenye asili ya Kigiriki na kubishana nao, wao waliamua kumwua. 30 Waamini wengine walipo pata habari hizi walimchukua hadi Kaisaria wakamsafirisha kwenda Tarso. 31 Ndipo kanisa katika Yudea yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Kanisa likapata nguvu likienenda katika kicho cha Bwana; na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.

Petro Amponya Ainea

32 Petro alipokuwa akiwatembelea waamini sehemu mbalimbali alifika kwa watu wa Mungu walioishi huko Lida. 33 Akamkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya; inuka utandike kitanda chako.” Na mara Ainea akainuka. 35 Wakazi wote wa Lida na Sharoni wali pomwona Ainea akitembea walimgeukia Bwana.

Petro Amfufua Dorkasi

36 Huko Jopa kulikuwa na mwanafunzi mwanamke aliyeitwa Tabita au kwa lugha ya Kigiriki, Dorkasi, yaani paa. Huyu mama alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37 Hata hivyo aliugua akafa. Wakamwosha na kumlaza katika chumba cha ghorofani. 38 Kwa kuwa Jopa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kuwa Petro yuko Lida, waliwatuma wenzao wawili wakamwambie, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39 Kwa hiyo Petro akaharakisha akaenda nao Jopa. Alipowasili wakampeleka hadi kwenye chumba alipokuwa amelazwa marehemu Dor kasi. Wajane wengi walikuwa wamemzunguka marehemu wakilia na kuonyesha mavazi ambayo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa hai. 40 Petro akawatoa wote nje, kisha akapiga magoti akaomba; akaugeukia ule mwili akasema, “Tabita, Amka!” Dorkasi akafumbua macho na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamsaidia kusimama. Ndipo alipowaita wale waamini na wajane aka wakabidhi Dorkasi akiwa hai. 42 Habari hizi zilienea sehemu zote za Jopa. Na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Petro akakaa Jopa kwa muda mrefu, akiishi na mtengenezaji ngozi mmoja aitwaye