Mashtaka Ya Wayahudi Juu Ya Paulo
1Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akafika pamoja na baadhi ya wazee na wakili mmoja aitwaye Tertulo. Wakatoa mashtaka yao juu ya Paulo mbele ya Gavana. 2 Na Paulo alipoitwa, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akasema, “Mtukufu Feliksi, kutokana na uongozi wako wa busara tumekuwa na amani ya kudumu na tunatambua ya kuwa mabadiliko mengi muhimu yaliyotokea katika taifa letu yameletwa na uwezo wako wa kuona mbele. 3 Wakati wote na kila mahali tunapokea mambo haya yote kwa shukrani za dhati. 4 Lakini nisije nikakuchosha, nakuomba kwa hisani yako utusikilize kwa muda mfupi. 5 Tumemwona mtu huyu kuwa ni mfanya fujo ambaye ana chochea maasi kati ya Wayahudi dunia nzima. Yeye ni kiongozi wa dhehebu la Wanazareti. 6 Tena alijaribu kulichafua Hekalu letu lakini tulimkamata [tukataka kumhukumu kwa mujibu wa sheria zetu, 7 lakini jemadari Lisia alikuja akamchukua kutoka kwetu kwa kutu mia nguvu 8 akaamuru wanaomshtaki walete mashtaka yao mbele yako]. Wewe mwenyewe ukimwuliza maswali utathibitisha ukweli wa mashtaka yote tunayoleta mbele yako kumhusu yeye.” 9 Wayahudi wakamwunga mkono wakithibitisha kwamba mashtaka yote yalikuwa ya kweli.
Paulo Ajitetea Mbele Ya Feliksi
10 Gavana Feliksi alipomruhusu Paulo ajitetee, yeye alisema, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi kwa hiyo natoa utetezi wangu bila wasi wasi. 11 Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipokwenda Yerusalemu kuabudu. 12 Hawa wanaonish taki hawakunikuta nikibishana na mtu ye yote au nikianzisha fujo katika Hekalu au katika sinagogi au mahali pengine po pote mjini. 13 Wala hawawezi kabisa kuthibitisha mambo haya wanayon ishtaki. 14 Lakini nakiri mbele yako kuwa mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kwa kufuata ile ‘Njia’ ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kilichoandikwa katika Sheria ya Musa na Mana bii 15 na ninalo tumaini kwa Mungu ambalo hata na wao wanaliku bali, kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote, walio na haki na wasio na haki. 16 Kwa hiyo ninafanya kila jitihada kuishi nikiwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 17 Basi, baada ya kuwa nje ya Yerusalemu kwa miaka kadhaa nilikuja mjini kuwale tea watu wa taifa langu sadaka kwa ajili ya maskini na kutoa dha bihu. 18 Nilikuwa nimeshatakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya, na hapakuwa na umati wa watu wala fujo yo yote. 19 Lakini kulikuwa na Wayahudi kutoka Asia, nadhani nao walista hili wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka yao kama wanalo lo lote la kunishtaki. 20 La sivyo, watu hawa waseme ni kosa gani walilogundua nimefanya niliposhtakiwa mbele ya Baraza, 21 isipo kuwa lile jambo nililotangaza wazi wazi nilipojitetea mbele yao, kwamba, ‘Mimi nimeshtakiwa mbele yenu leo kuhusu ufufuo wa wafu.’
22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.” 23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia. 24 Baada ya siku chache Feliksi akaja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Akatuma Paulo aitwe, wakamsikiliza akizungumza juu ya kumwamini Kristo Yesu. 25 Na Paulo alipokuwa akiwaeleza juu ya kuwa na kiasi na juu ya hukumu ya mwisho, Feliksi aliin giwa na hofu akasema, “Tafadhali sasa nenda, nitakuita tena nikipata nafasi.” 26 Wakati huo huo Feliksi alitazamia kwamba Paulo angempatia hongo, kwa hiyo akawa anamwita mara kwa mara kuzungumza naye. 27 Lakini baada ya miaka miwili kupita, Porkio Festo akachukua nafasi ya Feliksi kama Gavana; na kwa sababu Feliksi alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, akamwacha Paulo gere zani.