Malaika Amtoa Petro Gerezani
1Wakati huu mfalme Herode aliwatesa vikali baadhi ya waamini katika kanisa. 2 Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 3 Alipoona kuwa kitendo hicho kimewapendeza Wayahudi, akaamuru Petro akamatwe. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu. 4 Baada ya kumkamata Petro walimweka jela chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, kila kikundi kikiwa na askari wanne. Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro mbele ya Wayahudi baada ya Pasaka. 5 Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani; lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii. 6 Usiku ule ambao Herode alikuwa ameamua kumtoa kwa watu, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa kwa minyororo miwili, na askari wengine walikuwa wakilinda nje ya lango la gereza. 7 Mara malaika wa Bwana akatokea, na mwanga ukamulika ndani ya chumba. Yule malaika akampiga Petro ubavuni akamwamsha, akisema, “Haraka! Amka!” Na mara ile minyororo ikaanguka toka mikononi mwa Petro. 8 Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Vaa koti lako unifuate.” 9 Petro alitoka mle gere zani akifuatana na malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitokea yalikuwa kweli. Alidhani alikuwa katika ndoto. 10 Wal ipita kituo cha askari wa kwanza, na kituo cha askari wa pili, ndipo wakafika katika lango la chuma la kutokea kuelekea mjini. Lango likafunguka lenyewe, wakatoka nje wakaelekea katika bara bara mojawapo . Mara yule malaika akamwacha Petro. 11 Ndipo Petro alipopata fahamu sawa sawa, akasema, “Sasa nina hakika ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake aniokoe kutoka kwa Herode na maovu yote ambayo Wayahudi walikuwa wamekusudia kunitendea.”
12 Baada ya kutambua alipokuwa, Petro alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana Marko, ambako waamini wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 13 Petro alipobisha hodi mlangoni, mfany akazi msichana aitwaye Roda, akaja kumfungulia.
4 Lakini ali potambua sauti ya Petro, alirudi mbio kwa furaha kuwaambia wen gine kuwa Petro yuko nje, hata akasahau kumfungulia . 15 Wakam wambia yule msichana, “Una kichaa!” Lakini yeye alisisitiza kwamba ilikuwa ni kweli amesikia sauti ya Petro. Wakasema, “Ni malaika wake.” 16 Wakati huo Petro aliendelea kugonga mlangoni; nao walipofungua mlango wakamwona Petro, walistaajabu sana. 17 Lakini yeye aliwaashiria wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa jela. Akawaambia, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Akaondoka akaenda sehemu nyingine. 18 Kulipopam bazuka kukawa na hekaheka huko gerezani. Askari wakawa wanauli zana kuhusu yaliyompata Petro. 19 Herode akaamuru msako ufanyike lakini waliposhindwa kumpata Petro, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri hao askari wauawe. Basi Herode akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko.
Kifo Cha Herode
20 Herode alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakapeleka wajumbe wakaonane na Herode. Wajumbe hao wakapata kibali cha Blasto, mtumishi mwaminifu wa Mfalme Herode, ili waonane na mfalme kutaka amani kwa kuwa miji hiyo ilipata chakula chake kutoka katika milki ya mfalme. 21 Siku ya hao wajumbe kumwona mfalme ilipofika, Herode alivaa mavazi rasmi ya kifalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi akaanza kutoa hotuba. 22 Alipokuwa akihutubu watu walimshangilia, wakapiga kelele wakisema, “Hii ni sauti ya Mungu! Sio sauti ya mwanadamu!” 23 Mara malaika wa Bwana akampiga Herode; akaliwa na funza akafa kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. 24 Lakini neno la Mungu liliendelea kuenea na waamini wakaongezeka sana. 25 Barnaba na Sauli walipomaliza kazi yao walirudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana Marko.