Filemoni

1Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, pamoja na ndugu yetu Timotheo. Tunakuandikia wewe Filemoni mfanyakazi mwenzetu mpendwa, na dada yetu Afia na askari mwenzetu Arkipo, 2pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwako 3Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu

Upendo Na Imani Ya Filemoni

4Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapokuombea 5kwa sababu ninasikia habari za upendo wako na imani uliyonayo kwa Bwana wetu Yesu na kwa watakatifu wote. 6Ninakuombea kwamba unaposhirikiana na wengine juu ya imani yako upate kuelewa kikamilifu kila jambo jema ambalo tunapata ndani ya Kristo. 7Ndugu yangu, upendo wako umenipa furaha kubwa na faraja, kwa maana wewe umechangamsha mioyo ya watakatifu.

Ombi Kuhusu Onesmo

8Kwa sababu hii, ingawa nina ujasiri ndani ya Kristo kuku amuru ufanye linalotakiwa, 9lakini kwa ajili ya upendo, ninaona ni bora zaidi nikuletee ombi. Mimi Paulo, balozi ambaye sasa ni mfungwa kwa ajili ya Yesu Kristo, 10ninalo ombi kwako kuhusu mwanangu Onesmo; ambaye nimekuwa baba yake wa kiroho nikiwa gere zani. 11Hapo awali huyu Onesmo alikuwa hakufai, lakini sasa amekuwa wa manufaa kwako na kwangu pia.

12Ninamrudisha kwako, yeye ambaye ni kama moyo wangu mwe nyewe. 13Ningelipenda akae nami hapa anisaidie badala yako wakati huu ambapo niko gerezani kwa ajili ya Injili. 14Lakini sikupenda kufanya lo lote pasipo wewe kuniruhusu maana sipendi unisaidie kwa kulazimishwa, bali kwa hiari yako mwenyewe.

15Pengine Onesmo aliondoka kwako kwa muda mfupi kusudi uta kapompata tena uweze kuwa naye daima; 16na asiwe tena kama mtumwa tu, bali kama ndugu mpendwa. Yeye ni wa thamani sana kwangu lakini hasa zaidi kwako, maana pamoja na kuwa mtumwa wako, sasa ni ndugu yako katika Bwana.

17Kwa hiyo ikiwa unanihesabu kama mshiriki mwenzako, basi mpokee kama vile ambavyo ungenipokea mimi. 18Kama amekukosea jambo lo lote au ana deni lako, basi unidai mimi. 19Mimi Paulo ninaandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe, nitalipa. Wala sidhani nina haja ya kukukumbusha kwamba wewe mwenyewe ni mdeni wangu kwa ajili ya nafsi yako. 20Kwa hiyo ndugu yangu, ninaamini utafanya jambo hili kwa ajili ya Bwana. Burudisha moyo wangu katika Kristo.

21Naandika nikiwa na hakika ya kuwa utatii ninalokuambia na kwamba utafanya hata zaidi ya haya. 22Tena nakuomba unitayar ishie chumba cha kukaa, kwa maana natarajia kurudi kwenu kama jibu la Mungu kwa maombi yenu.

23Salamu zenu kutoka kwa Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu; 24na kutoka kwa Marko, Aristarko, Dema na