Matendo Ya Mitume 18

Paulo Aenda Korintho

1Baada ya haya, Paulo aliondoka Athene akaenda Korintho. Huko alimpata Myahudi mmoja jina lake Akila, mzaliwa wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu mfalme Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona. Akakaa nao na kufanya kazi na Akila kwa sababu wote wawili walikuwa mafundi wa kutengeneza mahema. Kila siku ya sabato Paulo alikwenda katika sinagogi akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki waamini. Sila na Timotheo walipofika kutoka Makedonia walimkuta akihubiri na kuwashuhudia Wayahudi na Wagiriki, kuwa Yesu ndiye Kristo. Wal ipombishia na kumtukana alikung’uta mavazi yake akawaambia, “Mimi sina lawama, mkipotea , lawama iko juu yenu wenyewe. Tangu sasa nitawahubiria mataifa neno la Mungu.” Kwa hiyo Paulo akaondoka akaenda kwenye nyumba ya mtu anayeitwa Titio Yusto ali yekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa karibu sana na sinagogi. Kiongozi wa hilo sinagogi aliyeitwa Krispo akamwamini Bwana pamoja na jamaa yake; na Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa. Usiku mmoja Bwana akazungumza na Paulo katika ndoto akamwambia, “Usiogope, endelea kuhubiri wala usi kate tamaa. 10 Kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia na kukudhuru; kwa kuwa kuna watu wengi walio wangu katika mji huu.” 11 Kwa hiyo Paulo akakaa Korintho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, akiwafundisha waamini neno la Mungu. 12 Lakini wakati Galio alipofanywa kuwa Liwali wa Akaya, Wayahudi waliungana kumshambulia Paulo, Wakamkamata na kumpeleka Mahakamani. 13 Wakamshitaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria zetu.” 14 Paulo alipo taka kujitetea Galio akawaambia Wayahudi, “Kama mashtaka yenu yalihusu makosa ambayo mtu huyu amefanya au kama yangehusu ujam bazi, ningewasikiliza. 15 Lakini kwa kuwa kesi hii inahusu maneno na majina yaliyo katika sheria zenu, itawabidi muiamue wenyewe. Nakataa kabisa kujihusisha na jambo hili.” 16 Akawafu kuza kutoka mahakamani. 17 Wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya mahakama. Wala Galio hakuingilia kati.

Paulo Arudi Antiokia

18 Baada ya haya Paulo alikaa huko Korintho kwa siku nyingi zaidi kisha akaagana na wale ndugu waamini akasafiri kwa meli kuelekea Siria akiongozana na Prisila na Akila. Walipofika Kenk rea Paulo alinyoa nywele zake kwa maana alikuwa ameweka nadhiri. 19 Walipofika Efeso Paulo aliwaacha Prisila na Akila, akaenda katika sinagogi akawa akijadiliana na Wayahudi. 20 Walipomwambia akae nao kwa muda mrefu zaidi alikataa, 21 lakini alipokuwa aki waaga aliwaambia, “Nitarudi kama Mungu akipenda.” Akasafiri kwa meli kutoka Efeso. 22 Alipofika Kaisaria alikwenda kuwasalimu ndugu katika kanisa kisha akaelekea Antiokia. 23 Alikaa Antiokia kwa muda, na baadaye aliondoka akatembelea makanisa huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha waamini wote.

Apolo Ahubiri Efeso Na Korintho

24 Basi Myahudi mmoja jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksan dria alikuja Efeso. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhu biri na pia aliyajua Maandiko barabara. 25 Alikuwa amefundishwa njia ya Bwana naye akiwa amejaa moto wa kiroho alifundisha kwa usahihi juu ya Yesu. Lakini ujuzi wake uliishia kwenye ubatizo wa Yohana. 26 Apolo alihubiri kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27 Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28 maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.