Matendo Ya Mitume 28

28 Tulipofika salama nchi kavu, tuligundua kwamba tuko katika kisiwa kiitwacho Melita. Wenyeji wa kisiwa hicho walitufanyia ukarimu wa ajabu, wakawasha moto na kutukaribisha kwa maana mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi kali. Paulo alikuwa amekusanya kuni nyingi na alipokuwa akiziweka kwenye moto, aka toka humo nyoka mwenye sumu akikimbia ule moto akajisokotea kwe nye mkono wa Paulo. Wale wenyeji walipomwona yule nyoka ameji sokota kwenye mkono wa Paulo, wakaambiana, “Bila shaka mtu huyu ni muuaji, ijapokuwa ameokoka kufa maji baharini, haki haikumru husu aishi.” Lakini Paulo akamkung’utia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yo yote. Wakangojea wakitarajia kwamba atavimba au ataanguka ghafla na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na hawakuona dalili yo yote mbaya ikimto kea, wakabadili mawazo yao, wakasema yeye ni mungu.

Karibu na pwani ile, kulikuwa na shamba kubwa la gavana wa kisiwa kile aliyeitwa Publio. Huyu gavana alitukaribisha kwa ukarimu mkubwa, akatufanyia sherehe kwa muda wa siku tatu. Baba yake Publio alikuwa mgonjwa amelala, ana homa kali na kuhara damu. Paulo akaenda kumwona, akamwekea mikono akamwombea; naye akapona. Jambo hili lilipotokea, watu wote wa kisiwa kile wal iokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. 10 Kwa hiyo wakatuletea zawadi nyingi, nasi tulipokuwa tukijiandaa kuondoka walitupatia kila kitu tulichohitaji kwa ajili ya safari.

Paulo Anawasili Rumi

11 Baada ya miezi mitatu tuliondoka kwa meli iliyokuwa ime toka Aleksandria ikawa imetia nanga katika kisiwa cha Melita mpaka majira ya baridi yaishe. Meli hiyo ilikuwa na picha ya miungu pacha Kasta na Poluksi. 12 Kituo chetu cha kwanza kili kuwa Sirakusa ambako tulikaa kwa siku tatu. 13 Kutoka huko tuka zunguka tukafika Regio; na baada ya siku moja, upepo mkali uka vuma kutoka kusini, na siku ya pili tukafika Puteoli. 14 Na hapa tuliwakuta waamini ambao walitukaribisha tukae nao kwa siku saba. Ndipo tukaendelea na safari mpaka tukafika Rumi. 15 Ndugu waamini wa Rumi walipopata habari zetu, walikuja mpaka soko la Apio na wengine wakaja mpaka mahali paitwapo ‘Mikahawa Mitatu’ kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akachangamka. 16 Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda.

Paulo Ahubiri Rumi

17 Baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiy ahudi wa Roma na walipofika Paulo akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lo lote kuwadhuru watu wetu au kinyume cha mila za baba zetu, hata hivyo nilikamatwa Yerusalemu nikakabid hiwa kwa utawala wa Kirumi. 18 Wao walipokwisha kunihoji wali taka kuniachilia huru kwa sababu hawakuona kosa lo lote nililoli fanya linalostahili adhabu ya kifo. 19 Lakini Wayahudi walipinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ijapokuwa sikuwa na lalamiko lo lote juu ya taifa langu. 20 Hii ndio sababu nimeomba kuonana nanyi niwaeleze mambo haya. Kwa maana kusema kweli, nimevaa pingu hizi kwa sababu ya tumaini la Israeli.” 21 Wakamwambia, “Hatujapokea barua zo zote zinazoku husu wewe kutoka Yudea, wala hakuna ndugu ye yote aliyefika hapa ambaye ameleta ripoti mbaya kukuhusu. 22 Lakini tungependa kusi kia mawazo yako kwa sababu tunajua kwamba kila mahali watu wana zungumza mabaya kuhusu dhehebu hili.” 23 Basi wakapanga siku ya kumsikiliza, na ilipofika, wakaja watu wengi mahali alipokuwa anakaa Paulo. Akawaeleza kuhusu Ufalme wa Mungu tangu asubuhi hadi jioni, akijaribu kuwahakikishia juu ya Yesu akitumia Maan diko ya Musa na Manabii. 24 Baadhi yao wakakubali, wakaamini, lakini wengine wakakataa kuamini. 25 Kwa kuwa hawakukubaliana kati yao, wakaamua kuondoka, na walipokuwa tayari kuondoka, Paulo akawaambia, “Roho Mtakatifu alisema kweli alipowaambia baba zenu kupitia nabii Isaya: 26 ‘Nenda ukawaambie watu hawa, mtasikiliza na kusikiliza, lakini hamtaelewa. Mtatazama na kutazama lakini hamtatambua. 27 Kwa sababu mioyo ya watu hawa imepumbaa, masikio yao hayasikii na wamefunga macho yao. Kama si hivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa mioyo yao na kunigeukia; nami ningewaponya.’ 28 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa mataifa; wao wata sikiliza.” 29 Baada ya Paulo kusema maneno haya Wayahudi wakaondoka wakibishana vikali wao kwa wao.] 30 Kwa muda wa miaka miwili Paulo aliishi katika nyumba ya kupangisha akiwakaribisha wote waliokuja kumwona.