Anania Na Safira
1Pia mtu mmoja jina lake Anania na mkewe Safira waliuza mali yao. 2 Lakini Anania, kwa makubaliano na mkewe akaficha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobakia kwa mitume.
3 Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza , fedha ulizopata zilikuwa zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini akafa. Na wote waliosikia maneno haya wakajawa na hofu. 6 Vijana wakaingia wakaufunga mwili wake wakamchukua nje kumzika.
7 Na baada ya muda wa saa tatu mkewe Anania akaingia, naye hakuwa na habari ya mambo yaliyotokea. 8 Petro akamwuliza, “Niambie, je? Mliuza shamba lenu kwa kiasi hiki?” Akajibu, “Ndio, tuliuza kwa kiasi hicho.”
9 Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje wewe na mumeo mkaamua kumjaribu Roho Mtakatifu wa Bwana? Tazama, vijana waliomzika mumeo wako mlangoni nao watakuchukua nje.”
10 Na mara akaanguka chini akafa. Wale vijana walipoingia wakamwona kuwa amekufa, wakamchukua wakamzika karibu na mumewe. 11 Waamini wote na watu wote waliosikia habari hizi wakajawa na hofu kuu.
Mitume Wafanya Miujiza Mingi Na Maajabu
12 Mitume walifanya miujiza mingi na ishara za ajabu. Na waamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kujiunga nao lakini watu wote waliwaheshimu sana. 14 Hata hivyo watu wengi zaidi, wanaume kwa wanawake walikuwa wakiongezeka katika kundi la waliomwamini Bwana. 15 Hata walikuwa wakiwabeba wagonjwa wakawalaza kwenye mikeka barabarani ili Petro alipokuwa akipita kivuli chake kiwa guse angalau baadhi yao, wapone. 16 Pia watu walikusanyika kutoka katika miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu wakileta wagonjwa na watu waliopagawa na pepo wachafu, hao wote wakapo nywa.
Mitume Washitakiwa
17 Kuhani mkuu na wale waliomuunga mkono, yaani Masadukayo, walijawa na wivu, 18 wakawakamata mitume na kuwatia gerezani.
19 Lakini usiku ule malaika wa Bwana akaja akawafungulia milango ya gereza akawatoa nje akawaambia, 20 “Nendeni mkasi mame Hekaluni mkawaambie watu habari za maisha haya mapya!”
21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaanza kufundisha watu. Kuhani Mkuu alipowasili pamoja na wenzake wakaitisha mkutano wa baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. 22 Lakini wale maafisa wal iotumwa walipoingia gerezani hawakuwakuta wale mitume mle. Kwa hiyo wakarudi kutoa ripoti kwa baraza. 23 Wakasema, “Tumekuta milango ya jela imefungwa sawasawa, na maaskari wa gereza wamesi mama nje ya milango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu ye yote ndani.”
24 Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia ripoti hiyo wakashangaa sana wasijue mambo haya yan geishia wapi. 25 Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Wale watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.”
26 Ndipo yule mkuu wa kikosi cha walinzi wa Hekalu na wale maofisa wakaenda wakawaleta mitume lakini hawakuwadhuru kwa sababu waliogopa wangelipigwa mawe na watu. 27 Baada ya kuwaleta wakawaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu akaanza kuwahoji,
28 “Tuliwakanya msifundishe kwa jina la huyu mtu, lakini ninyi mmeeneza mafundisho yenu Yerusalemu yote, na tena mmeamua kuwa sisi tuna hatia juu ya kifo chake.”
29 Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu na sio wanadamu. 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu ambaye ninyi mlimwua kwa kumtundika kwenye msalaba. 31 Mungu alimwinua, akamweka mkono wake wa kuume awe Mtawala na Mwokozi ili awape wana wa Israeli toba na msamaha wa dhambi. 32 Nasi tu mashahidi wa mambo haya pamoja na Roho Mtakatifu aliyetolewa na Mungu kwa watu wanaomtii.”
Mungu kwa watu wanaomtii.”
33 Wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua wale mitume. 34 Lakini mmoja wao, Far isayo aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria aliyeh eshimiwa na watu wote, akasimama akaamuru wale mitume watolewe nje kwa muda.
35 Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Wazee wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mtakalowatendea watu hawa! 36 Kumbukeni kuwa sio zamani sana tangu alipotokea mtu aliyeitwa Theuda ambaye alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi mia nne wal ioambatana naye. Lakini aliuawa na wafuasi wake wote wakatawany ika, kazi yake ikawa bure. 37 “Baada yake alitokea Yuda Mgali laya wakati ule wa sensa, akapata wafuasi wengi; lakini naye akauawa nalo kundi lake likatawanyika.
38 “Kwa hiyo, kwa kesi hii nawashauri waacheni watu hawa wala msiwatendee lo lote, kwa maana kama mpango wao na kazi yao ni mambo ya wanadamu hayatafika po pote; 39 lakini ikiwa ni kazi ya Mungu hamtaweza kuwazuia. Badala yake huenda mkajikuta mnam pinga Mungu!”
40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli; wakawaita mitume ndani na baada ya kuwachapa viboko wakawaamuru wasifundishe kwa jina la Yesu. Wakawaachia waende zao. 41 Wale mitume walitoka barazani wamejaa furaha kwa sababu Mungu aliwapa heshima ya kupata aibu ya kuchapwa viboko kwa ajili ya jina la Yesu. 42 Na kila siku Hek aluni na nyumbani walizidi kuhubiri na kufundisha bila kukoma, juu ya Habari Njema kwamba Yesu ndiye Kristo.