1 1 0Wakati alipokuwa akifukiza uvumba umati mkubwa wa watu walikuwa nje wakiomba. 2wakitumia maelezo ya wale wal ioshuhudia mambo haya kwa macho yao na wale waliotabiri habari hizo. 3Lakini, mimi pia, nimezichunguza habari hizi kuanzia mwanzo. Nami nimeona ni vema nikuandikie kwa mpango, muhtasari huu, 4ili upate kuwa na hakika ya mambo yote uliyofundishwa.
Utabiri Kuhusu Yohana Mbatizaji
5Historia ya mambo haya ilianzia katika jamaa ya kuhani mmoja Myahudi aliyeitwa Zakaria. Yeye aliishi wakati Herode ali pokuwa mfalme wa Yudea na alihudumu katika kikundi cha ukuhani cha Abia. Mkewe Zakaria aliitwa Elizabeti naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. 6Zakaria na Elizabeti walikuwa watu wenye kumcha Mungu, wakitii amri zake zote na kutimiza maagizo yake yote kika milifu. 7Lakini hawakuwa na watoto, maana Elizabeti alikuwa tasa; na wote wawili walishapita umri wa kuzaa. 8-9 Siku moja, kikundi cha Zakaria kilikuwa na zamu Hekaluni na Zakaria alikuwa anafanya huduma yake ya ukuhani kwa Mungu. Walipopiga kura, kama ilivyokuwa desturi, ili wamchague atakayeingia kufukiza uvumba madhabahuni, Zakaria alichaguliwa. 11Ghafla, malaika wa Bwana akamtokea Zakaria. Akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia uvumba. 12Zakaria alipomwona huyo mal aika alishtuka akajawa na hofu.
13Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria! Kwa maana Mungu amesikia maombi yako, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana. 14Nawe utakuwa na furaha kubwa moyoni wakati huo na watu wengi watashangilia kuzaliwa kwake. 15Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana, hataonja divai wala kinywaji cho chote cha kulevya; atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. 16Naye atawavuta Wayahudi wengi warudi kwa Bwana, Mungu wao. 17Yeye atamtangulia Bwana akiongozwa na Roho na nguvu ya nabii Eliya. Atawapatanisha akina baba na watoto wao. Atawarejesha waasi katika njia ya wenye haki na kuandaa watu wa Bwana kwa ajili ya kuja kwake.” 18Zakaria akamwambia mal aika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa!” 19Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu. Yeye ndiye aliyenituma kwako nikuambie habari hizi njema. 20Sikiliza! Kwa sababu huku niamini, utakuwa bubu, hutaweza kusema mpaka maneno yangu yataka pothibitishwa wakati mtoto huyo atakapozaliwa.” 21Wakati mambo haya yakitokea mle Hekaluni, watu waliokuwa nje wakimngojea Zakaria walikuwa wakishangaa kwa nini alikawia kutoka. 22Hati maye alipotoka hakuweza kusema nao. Wakatambua ya kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Kwa kuwa alikuwa bubu, akawaashiria kwa mikono. 23Muda wake wa zamu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24Kisha baada ya muda si mrefu, Elizabeti mkewe alipata mimba, naye akajificha kwa miezi mitano akisema: 25“Bwana amekuwa mwema kwangu. Maana ameniondolea aibu yangu mbele za watu.”
Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa
26Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.
28Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
29Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”
34Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?” 35Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu ata kujilia na nguvu za Mungu zitakufunika kama kivuli, na kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu na ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tena, miezi sita iliyopita binamu yako Elizabeti, aliyeitwa tasa, amepata mimba ingawa ni mzee sana. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”
38Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.’ ’ Kisha malaika akaondoka.
Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti
39, 40Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti. 41Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa. 43Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu! 44Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha. 45Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.” 46Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana, 47na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 48Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa. 49Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu. 50Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao. 51Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya. 52Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge. 53Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54Amem saidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake, 55kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.” 56Mar iamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.
Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji
57Ikawa siku za kujifungua kwake Elizabeti zilipotimia, alizaa mtoto wa kiume . 58Habari zikawafikia majirani na jamaa jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu. Nao wakafurahi pamoja naye. 59Mtoto alipokuwa na umri wa siku nane, watu wakaja kuhudhuria tohara yake. Wote wakataka wampe yule mtoto jina la Zakaria, yaani jina la baba yake. 60Lakini mama yake akakataa na kusema, “La si hilo. Jina lake litakuwa Yohana.” 61Wakamjibu, “Mbona hakuna mtu katika jamaa yako mwenye jina kama hilo?” 62Basi wakaamua kumwuliza Zakaria kwa ishara kwamba yeye angependa mtoto aitwe nani. 63Akaomba mahali pa kuandikia, naye akaandika: “Jina lake ni Yohana.” Watu wote wakastaajabu. 64Papo hapo uwezo wa kusema ukamrudia Zakaria naye akaanza kumsifu Mungu. 65Watu wote walioshuhudia jambo hili wakastaajabu mno, na habari hii ikaenea sehemu zote za wilaya ile ya Yudea. 66Na kila aliyezisikia habari hizi aliwaza moyoni: “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Utabiri Wa Zakaria
67Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akata biri akisema: 68“Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake ili awakomboe. 69Naye ametusimamishia nguvu ya wokovu katika ukoo wa Daudi mtumishi wake; 70kama alivy oahidi kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani: 71kwamba atatuokoa na maadui zetu na kututoa kutoka katika mikono ya wote watuchukiao. 72Aliahidi ataonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu 73aliloagana na baba yetu Ibrahimu: 74kutuokoa kutoka katika mikono ya adui zetu na kutuwezesha kumtumikia pasipo woga, 75katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. 76Na wewe mwanangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia Bwana na kumwandalia njia; 77na kuwafahamisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, 78kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na 79kuwaangazia wote waishio katika giza na katika uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” 80Yule mtoto akakua na kuko maa kiroho; akaishi nyikani hadi alipoanza kuwahubiria Waisraeli hadharani.