1Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wathes alonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. 2Tuna watakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.
Sala Na Shukrani
3Hatuna budi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu wapendwa; na ndivyo inavyostahili kwa sababu imani yenu inaongezeka zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu kwa mwen zake unazidi kuongezeka. 4Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tunajivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazopata.
5Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake. 6Mungu ni wa haki: atawalipa kwa mateso wale wanaowatesa ninyi 7na kuwapeni ninyi mnaoteseka nafuu pamoja na sisi pia. Haya yatatokea wakati Bwana Yesu atakapodhi hirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, 10siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabiwa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa mion goni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
11Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. 12Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.