Mungu Ajibu Sala Ya Kornelio
1Katika mji wa Kaisaria aliishi afisa mmoja wa jeshi ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha Italia, jina lake Kornelio. 2 Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na jamii yake yote. Alitoa msaada kwa ukarimu kwa watu na kumwomba Mungu mara kwa mara.
3 Alasiri moja, mnamo saa tisa, malaika wa Mungu alimjia katika ndoto na kumwita, “Kornelio!” 4 Kornelio akamtazama yule malaika kwa hofu akasema, “Ni nini Bwana?” Malaika akasema, “Sala zako na sadaka ulizotoa kwa maskini zimefika mbinguni, na Mungu amezikumbuka. 5 Sasa tuma watu Jopa wakamlete Simoni ait waye Petro. 6 Yeye hivi sasa anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi kando ya bahari.” 7 Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye ali poondoka, Kornelio aliwaita watumishi wake wawili na mlinzi wake mmoja aliyekuwa mcha Mungu, 8 na baada ya kuwasimulia mambo yote yaliyotokea, akawatuma waende Jopa.
9 Kesho yake, walipokuwa wanaukaribia mji, Petro alipanda juu ghorofani kuomba mnamo saa sita. 10 Alipokuwa akisali aliona njaa akatamani kupata chakula. Lakini wakati kilipokuwa kinaan daliwa, alisinzia akaota ndoto. 11 Akaona katika ndoto mbingu zimefunguka na kitu kama shuka kubwa ikishushwa kwa ncha zake nne. 12 Ndani ya ile shuka walikuwemo aina zote za wanyama na nyoka na ndege. 13 Kisha sauti ikamwambia Petro, “Inuka, uchinje na ule mnyama ye yote umpendaye kati ya hawa.” 14 Petro akajibu, “La Bwana! Sijawahi kula cho chote ambacho kimetajwa na sheria zetu za Kiyahudi kuwa ni kichafu.” 15 Ile sauti ikarudia kusema naye mara ya pili, “Usiite cho chote alichokitakasa Bwana kuwa ni kichafu.” 16 Hii ilitokea mara tatu, ndipo ile shuka ikarudishwa mbinguni.
17 Petro alikuwa bado akijiuliza maana ya mambo haya aliyoy aona, wakati wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio walipofika kwenye nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi. 18 Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.
19 Wakati huo Petro alikuwa akifikiria juu ya ile ndoto, Roho Mtakatifu akamwambia, “Wako watu watatu wamekuja kukuta futa. 20 Shuka chini ukaonane nao na usione shaka kwenda nao kwa kuwa nimewatuma kwako.” 21 Petro akashuka, akawaendea wale watu akawaambia, “Mimi ndiye mnayemtafuta. Mnataka nini?” 22 Wao wakamjibu, “Tumetumwa na Kamanda Kornelio ambaye ni mtu mwema anayemcha Mungu na kusifiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagi zwa na malaika wa Mungu akukaribishe nyumbani kwake, ili asiki lize maneno utakayomwambia.” 23 Petro aliwakaribisha walale kwake. Kulipokucha akaandamana nao pamoja na baadhi ya ndugu waamini wa pale Jopa.
Petro Nyumbani Kwa Kornelio
24 Kesho yake wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwan goja pamoja na ndugu zake na marafiki wa karibu ambao alikuwa amewaalika. 25 Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akapiga magoti. 26 Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama! Mimi ni mwanadamu tu.” 27 Petro alipokuwa akizungumza naye aliingia ndani ambapo alikuta watu wengi wamekusanyika. 28 Petro akawaambia, “Mnajua kwamba sheria ya Wayahudi hairu husu Myahudi kuwatembelea au kuchangamana na watu wa mataifa men gine kama hivi nifanyavyo. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwone mtu ye yote kuwa mchafu au asiyefaa. 29 Ndiyo sababu ulipotuma nije sikusita. Kwa hiyo naomba unieleze kwa nini ume niita.” 30 Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa mchana. Mara akatokea mtu aliyevaa nguo za kung’ara akasimama mbele yangu. 31 Akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na Mungu, naye amekumbuka msaada wako kwa maskini. 32 Basi tuma watu waende Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. Yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko sehemu za pwani.’ 33 Ndio sababu nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vizuri kuja. Basi sasa tuko hapa wote mbele ya Mungu kuyasikiliza yote ambayo Mungu amekuamuru kutuambia.”
Hotuba Ya Petro
34 “Ndipo Petro alianza kwa kusema, “Sasa naamini ya kuwa Mungu hana upendeleo. 35 Yeye huwakubali watu wa kila taifa wam chao na kutenda haki. 36 Huu ndio ujumbe ambao Mungu aliwapele kea watu wa Israeli, kuhusu Habari Njema za amani kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wa wote. 37 Ninyi bila shaka mnafa hamu mambo yaliyotokea sehemu zote za Yudea, kuanzia Galilaya tangu wakati wa mahubiri ya Yohana Mbatizaji. 38 Mnafahamu jinsi Mungu alivyompa Yesu wa Nazareti Roho Mtakatifu na uwezo, na jinsi alivyozunguka kila mahali akifanya mema na kuponya wote waliokuwa wakiteswa na nguvu za shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyofanya katika nchi ya Wayahudi na Yerusalemu. Walimwua kwa kumtundika msalabani. 40 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu. 41 Hakuonekana kwa watu wote, lakini alionekana kwa mashahidi ambao Mungu aliwachagua, yaani sisi ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake. 42 Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote, na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwahukumu walio hai na wafu. 43 Manabii wote walishuhudia juu yake, kwamba kila mtu amwami niye atasamehewa dhambi katika jina lake.”
Mataifa Wapokea Roho Mtakatifu
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo, Roho Mtakatifu ali washukia wote waliokuwa wakisikiliza. 45 Wale Wayahudi waamini waliokuwa wamekuja na Petro walishangaa sana kuona kuwa Mungu aliwapa watu wa mataifa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa kuwa waliwasikia wakisema kwa lugha mpya na kumtukuza Mungu kwa ukuu wake. Ndipo Petro akasema, 47 “Je, kuna mtu anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” 48 Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.