1Kutoka kwa Simoni Petro mtumishi na mtume wa Yesu Kristo. Kwa wote ambao wamepokea imani yenye thamani kama yetu kutokana na haki ya Mungu wetu na Mwokozi Yesu Kristo.
2Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu
Wito Wa Kuishi Maisha Ya Kikristo
3Uweza wake wa kimungu umetupatia mambo yote yanayohusiana na uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake. 4Kwa njia hiyo ametupatia ahadi zake kuu na za tha mani. Mkishika ahadi hizo mtashiriki asili yake ya kimungu na kuepuka uovu ambao uko duniani kwa sababu ya tamaa mbaya.
5Kwa sababu hii, jitahidini sana kuongeza wema katika imani yenu; na katika wema ongezeni maarifa; 6na katika maarifa ongezeni kiasi; na katika kiasi ongezeni ustahimilivu; na katika ustahimilivu ongezeni kumcha Mungu; 7na katika kumcha Mungu ongezeni upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu ongezeni upendo. 8Maana mkiwa na sifa hizi kwa wingi zitawawe zesha kuwa wenye bidii na wenye kuzaa matunda katika kumfahamu Bwana wetu Yesu Kristo. 9Lakini mtu asiyekuwa na sifa hizi ni kipofu, haoni mbali, na amesahau kuwa ametakaswa dhambi zake za zamani.
10Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuhakikisha wito wenu na uteule wenu, kwa maana mkifanya hivyo, hamtaanguka kamwe; 11na mtakaribishwa kwa fahari kubwa katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Unabii Wa Maandiko
12Kwa hiyo ninakusudia kuwakumbusha hayo siku zote, ingawa mnayafahamu na mmekuwa imara katika kweli mliyo nayo. 13Nadhani ni vema niwahimize kwa kuwakumbusha mambo haya, wakati wote nina poishi katika mwili huu. 14Kwa maana najua kwamba karibu nitauweka kando mwili wangu, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyon ionyesha wazi. 15Na nitahakikisha kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaendelea kukumbuka mambo haya kila wakati.
16Tulipowafundisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulish uhudia kwa macho yetu utukufu wake. 17Maana alipopewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, na sauti ikamjia katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye’ 18tuliisikia sauti hii iliyotoka mbinguni, maana tulikuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.
19Kwa hiyo tuna uhakika zaidi juu ya ujumbe wa manabii. Hivyo itakuwa vema mkizingatia ujumbe huo, kama vile watu wanavy oitegemea taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka Siku ile itakapo fika na nyota ya asubuhi itakapoangaza mioyoni mwenu. 20Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe. 21Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.