Matendo Ya Mitume 6

Uchaguzi Wa Wahudumu

1Siku hizo, wakati idadi ya waamini ilipokuwa ikiongezeka sana palitokea manung’uniko. Wayahudi walioongea lugha ya Kigi riki walilalamika kuwa wakati wa kugawa chakula, wajane walioon gea Kiebrania walipendelewa na wajane wao walibaguliwa. Wale mitume kumi na wawili waliitisha kikao cha wanafunzi wote, wakasema, “Si sawa sisi tuache kazi ya kuhubiri neno la Mungu tuanze kugawa chakula. Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba mion goni mwenu; watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ili tuwakabidhi kazi hii. Na sisi tutatumia wakati wetu kwa kuomba na kufundisha neno la Bwana.”

Uamuzi huu ukawaridhisha wote nao wakawachagua Stefano, mtu aliyejawa na imani na Roho Mtakatifu; na Filipo, Prokoro, Nika nori, na Timoni, Parmena na Nikolao mwongofu wa kutoka Antiokia. Wakawaleta watu hawa mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono juu yao.

Na neno la Mungu likazidi kuenea; idadi ya wanafunzi ika zidi kuongezeka sana katika Yerusalemu, na hata makuhani wengi wakamwamini Yesu.

Stefano Akamatwa

Na Stefano akiwa amejawa na neema na nguvu za Mungu alifa nya maajabu makubwa na ishara kati ya watu.

Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa la ‘Watu Huru,’ na wengine kutoka masinagogi ya Kirene na Aleksandria, pamoja na baadhi kutoka Kilikia na Asia, wakajaribu kubishana na Stefano. 10 Lakini hawakuweza kushindana naye kwa sababu ya hekima yake na Roho aliyemwezesha kusema.

11 Ndipo wakawashawishi watu fulani ambao walisema, “Tulim sikia akisema maneno ya kufuru juu ya Musa na Mungu.”

Stefano Afikishwa Mbele Ya Baraza

12 Wakawachochea watu, wazee na waandishi wa sheria nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza. 13 Wakaweka mashahidi wa uongo ambao walisema, “Mtu huyu siku zote anasema maneno ya kashfa juu ya Hekalu hili takatifu na juu ya sheria za Musa. 14 Kwa maana tumemsikia akisema kwamba eti huyu Yesu wa Nazareti ataharibu hili Hekalu takatifu na atabadilisha mila zote tulizopewa na Musa.” 15 Watu wote waliokuwa katika baraza hilo walimtazama Stefano kwa makini wakaona uso wake unang’aa kama uso wa malaika! Hotuba Ya Stefano