1Kutoka kwa Paulo, aliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo, na Sosthene ndugu yetu.
2Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wote waliota kaswa katika Kristo Yesu, wakaitwa wawe watakatifu, pamoja na wengine wote ambao kila mahali wanalikiri jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wao na Bwana wetu. 3Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Baraka Zitokazo Kwa Kristo
4Ninamshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema aliyowapa ndani ya Kristo Yesu. 5Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kunena kwenu, katika maarifa yote, 6kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. 7Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8Yeye atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.
Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa
10Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane ninyi kwa ninyi, na pasiwepo na utengano kati yenu. Muungane pamoja kikamilifu katika kuwaza na katika kuamua. 11Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa watu wa nyumbani kwa Kloe kwamba kuna ugomvi kati yenu. 12Maana yangu ni kwamba: mmoja wenu anasema, “Mimi ni wa Paulo,” mwin gine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”
13Je, Kristo amegawanyika? Je, ni Paulo aliyewafia msala bani? Au mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14Namshukuru Mungu kwa sababu sikumbatiza mtu ye yote isipokuwa Krispo na Gayo. 15Kwa hiyo hakuna mtu kati yenu anayeweza kusema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16Ndiyo nakumbuka, pia niliwabatiza Stefano na watu wa nyumbani kwake. Lakini zaidi ya hao sikumbuki kama nilimbatiza mtu mwingine. 17Kwa maana Kristo hakunituma kubatiza bali kuhu biri Injili na nifanye hivyo pasipo kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu, ili nguvu ya kifo cha Kristo msalabani iwe dhahiri.
Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu
18Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19Maan diko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.” 20Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga? 21Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22Way ahudi wanataka ishara, Wagiriki wanatafuta hekima. 23Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa msalabani, ujumbe ambao ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa Wagiriki ni upuuzi. 24Lakini kwa walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
26Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa Mungu alipowaita. Si wengi mlikuwa na hekima kwa kipimo cha kibinadamu. Si wengi mli kuwa na vyeo na si wengi mlikuwa wa jamaa za kifahari. 27Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu. 28Mungu alichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa humu duniani, vitu ambavyo si kitu, ili avibatilishe vile ambavyo vinaonekana kuwa vya maana; 29ili mtu ye yote asijisifu mbele yake. 30Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi 31Kwa hiyo, kama Maan diko yasemavyo: “Mtu ye yote anayetaka kujisifu, basi ajisifu kwa ajili ya Bwana.”