Matendo Ya Mitume 8

1Na Sauli aliunga mkono kuuawa kwa Stefano Tangu siku hiyo waamini katika kanisa la Yerusalemu walianza kuteswa sana. Waamini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia katika majimbo ya Yudea na Samaria. 2Watu waliomcha Mungu walimzika Stefano na kumwombolezea sana. 3Lakini Sauli alitaka kulianga miza kanisa kabisa. Akawa akienda kila nyumba akawaburura waamini, wanaume kwa wanawake, akawatia jela.

Injili Yahubiriwa Samaria

4Wale waamini waliotawanyika walihubiri neno la Mungu kila mahali walipokuwa. 5Filipo naye alikwenda katika mji mmoja wa Samaria akahubiri habari za Kristo. 6Watu wengi walipomsikiliza Filipo na kuona ishara za ajabu alizofanya, walizingatia kwa makini ujumbe wake. 7Pepo wachafu walikuwa wakiwatoka watu wengi, huku wakipiga makelele; na wengi waliopooza na viwete, waliponywa. 8Pakawa na furaha kuu katika mji huo.

9Lakini katika mji huo alikuwepo mtu mmoja aitwaye Simoni, ambaye alikuwa mchawi. Kwa muda mrefu alikuwa amewapumbaza na kuwashangaza watu kwa mazingaombwe, akawa anajigamba kuwa yeye ni mtu maarufu. 10Watu wa tabaka zote, wakubwa kwa wadogo, walivu tiwa sana naye, wakawa wanasema, “Bila shaka mtu huyu ndiye ile nguvu ya Mungu iitwayo ‘Uwezo Mkuu.’ ” 11Wakamsikiliza kwa makini kwa sababu aliwastaajabisha kwa mazingaombwe yake. 12Lakini watu walipoamini mahubiri ya Filipo kuhusu Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, waume kwa wake. 13Hata Simoni naye aliamini na alipokwisha batizwa aliambatana na Filipo. Alipoona ishara na miujiza aliy ofanya Filipo alistaajabu sana .

14Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa watu wa Samaria wameamini neno la Bwana, waliwatuma Petro na Yohana waende huko. 15Nao walipofika waliwaombea ili wapokee Roho Mta katifu; 16kwa maana walikuwa wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu na Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia. 17Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao waka pokea Roho Mtakatifu. 18Simoni alipoona kuwa watu walipokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, aliwapa fedha 19akasema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apokee Roho Mtakatifu.” 20Petro akam jibu, “Uangamie wewe na fedha zako, kwa maana unadhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!” 21Wewe huwezi kuwa na sehemu wala fungu katika jambo hili kwa kuwa moyo wako hauko sawa mbele za Mungu. 22Kwa hiyo tubu, uache huu uovu wako; na umwombe Mungu ili kama inawezekana akusamehe makusudio maovu uliyo nayo moyoni. 23Kwa maana ninaona wazi kwamba wewe umejawa na wivu na ni mfungwa wa dhambi. 24Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Bwana, ili hayo mliyosema yasije yakanipata.” 25Nao wali pokwisha kutoa ushuhuda na kufundisha neno la Bwana, walirudi Yerusalemu; na walipokuwa wakisafiri walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.

Filipo Ambatiza Afisa Wa Ethiopia

26Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza.” Hii ilikuwa barabara iendayo jangwani. 27Filipo akaondoka akaenda. Wakati huo Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa Kandake, Malkia wa Ethiopia, alikuwa anarudi nyumbani baada ya kumwabudu Mungu huko Yerusalemu. 28Alikuwa amekaa kwenye gari la kuvutwa na farasi akielekea makwao, akisoma kitabu cha nabii Isaya. 29Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kasimame karibu na lile gari.” 30Kwa hiyo Filipo aka harakisha kulikaribia, na alipofika karibu akamsikia yule afisa akisoma katika kitabu cha nabii Isaya, akamwuliza, “Je, unaelewa unachosoma?” 31Yule afisa akamjibu, “Nitaelewaje mtu asipo nielekeza? Akamkaribisha Filipo katika gari, akaketi pamoja naye. 32Maneno aliyokuwa akisoma ni haya, ‘Alipelekwa kama kon doo anayetolewa kuchinjwa na kama mwana-kondoo anavyotulia anapo katwa manyoya, naye hakusema neno lo lote. 33Aliaibishwa, aka nyimwa haki yake. Ni nani awezaye kuelezea juu ya kizazi chake? Kwa maana uhai wake umeondolewa duniani.’ 34Yule towashi akam wuliza Filipo, “Tafadhali niambie, Isaya alikuwa akisema haya juu yake mwenyewe au juu ya mtu mwingine?” 35Ndipo Filipo akaanza kusema naye, akitumia Maandiko haya akamweleza Habari Njema za Yesu. 36Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, na yule towashi akamwambia Filipo, “ Tazama, hapa kuna maji! Kuna kitu gani cha kunizuia mimi nisiba tizwe? [ 37Filipo akamwambia, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”] 38Akaamuru gari lisimamishwe. Wakateremka, yule towashi na Filipo, wakaenda pale kwenye maji. Filipo akamba tiza. 39Walipotoka katika yale maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo na yule towashi hakumwona tena. Kwa hiyo akaendelea na safari yake akiwa amejawa na furaha. 40Filipo akajikuta yuko Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipo fika Kaisaria.