1Mfalme Agripa akamwambia Paulo, “Unayo ruhusa kujite tea.” Paulo akanyoosha mkono wake, akaanza kujitetea akasema,
2 “Mfalme Agripa, najiona kuwa mwenye bahati kwamba ninatoa utetezi wangu mbele yako kuhusu mashtaka yote ya Wayahudi. 3 Kwa sababu nafahamu ya kuwa wewe unajua kwa undani mila na maswala yote ya mabishano kati ya Wayahudi. Kwa hiyo nakusihi unisikilize kwa uvumilivu.
4 “Wayahudi wote wanajua jinsi nilivyoishi kutoka utotoni, kwa maana tangu mwanzo wa maisha yangu niliishi katika nchi yangu na pia Yerusalemu. 5 Pia wamefahamu wakati wote, na wanaweza kushuhudia, ya kuwa nililelewa na kuishi kama Mfarisayo nikifuata masharti halisi ya madhehebu ya dini yetu. 6 Na hata sasa nasi mama hapa nikiwa nashtakiwa kwa sababu nashikilia tumaini ambalo Mungu aliwaahidi baba zetu. 7 Ahadi hii ndio inawafanya makabila kumi na mawili ya Israeli wamwabudu Mungu kwa bidii usiku na mchana wakitarajia kuipokea. Mtukufu Mfalme, ni kwa ajili ya tumaini hili Wayahudi wamenishtaki! 8 Sijui ni kwa nini watu wanadhani ni jambo la ajabu lisilowezekana, kwamba Mungu anawafu fua wafu.
9 Mimi mwenyewe nilikuwa nimeamini kabisa kwamba sina budi kufanya kila niwezalo kupinga jina la Yesu wa Nazareti. 10 Nami ndivyo nilivyofanya kule Yerusalemu. Nilipewa mamlaka na makuhani wakuu, nikawatia kifungoni watakatifu wengi na walipokuwa wakihu kumiwa kuuawa mimi nilipiga kura kuunga mkono hukumu hiyo. 11 Pia niliwaadhibu mara nyingi katika masinagogi nikajaribu kuwalazimisha wakane imani yao. Nilikuwa nimejawa na ghadhabu juu yao nikawafuatilia na kuwatesa hata katika miji ya mbali.
12 “Nilikuwa katika mojawapo ya safari hizi nikielekea Dameski, nikiwa na kibali na amri kutoka kwa makuhani wakuu. 13 Mtukufu Mfalme, nilipokuwa njiani, mnamo saa sita mchana, niliona mwanga mkali kuliko wa jua kutoka mbinguni, ukaniangazia mimi na wale niliokuwa nao, pande zote. 14 Na wote tulipokuwa tumeanguka chini nilisikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kie brania, ‘Sauli, Sauli! Mbona unanitesa? Unajiumiza mwenyewe.’ 15 Nikauliza, ‘Ni nani wewe Bwana?’ Naye akasema, ‘Mimi ni Yesu unayenitesa. 16 Lakini sasa inuka usimame, kwa maana nimejidhi hirisha kwako ili nikuteue uwe mtumishi wangu, ukawaambie wengine mambo yote uliyoyaona kwangu leo, na yale nitakayokuonyesha baad aye. 17 Nitakuokoa kutoka kwa watu wako na watu wa mataifa. 18 Ninakutuma ukawafungue macho yao ili watoke kwenye giza waingie nuruni na watoke katika nguvu za shetani wamgeukie Mungu; ili wapokee msamaha wa dhambi na wapate nafasi pamoja na wote ambao wanatakaswa kwa kuniamini.’
19 Kwa hiyo mtukufu Agripa, sikuweza kuacha kutii haya maagizo ya maono kutoka mbinguni, 20 bali niliwahubiria kwanza watu wa Dameski kisha Yerusalemu na nchi yote ya Yudea na watu wa mataifa mengine pia. Niliwahimiza watubu dhambi zao wamgeukie Mungu na kuishi maisha yanayodhihirisha kwamba kweli wametubu. 21 Ni kwa sababu hii Wayahudi walinikamata nilipokuwa Hekaluni, wakataka kuniua. 22 Lakini mpaka wakati huu nimepata msaada uto kao kwa Mungu, na kwa hiyo nasimama hapa nikitoa ushuhuda wangu kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo. Nami sisemi lo lote ila yale ambayo Musa na manabii walitabiri yangetokea: 23 kwamba Kristo atateswa naye kwa kuwa atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, atatangaza mwanga wa wokovu kwa Wayahudi na watu wa mataifa.”
24 Paulo alipofikia hapa katika utetezi wake Festo aliin gilia kati akasema kwa sauti kubwa, “Paulo, umeehuka! Kusoma sana kumekufanya uehuke !” 25 Lakini Paulo akajibu, “Mimi si mwehu, Mtukufu Festo, bali nasema yale yaliyo kweli na ya kuami nika. 26 Mfalme Agripa anajua habari za mambo haya, ndio sababu najieleza wazi wazi mbele yake. Kwa sababu ninahakika kuwa yeye aliyaona mambo haya kwa kuwa hayakufichwa pembeni. 27 Mfalme Agripa, Unawaamini manabii? Ninajua kwamba unaamini.” 28 Kisha Agripa akamjibu, “Unadhani kuwa kwa muda huu mfupi unaweza kuni fanya nikubali kuwa mkristo!” 29 Paulo akasema, “Singejali kama ni kwa muda mfupi au mrefu, lakini shauku yangu ni kwamba wewe na wote wanaonisikiliza leo muwe kama mimi nilivyo, isipo kuwa tu hii minyororo.’ ’ 30 Ndipo Mfalme akasimama na Gavana na Bernike na wengine wote waliokuwa wameketi nao wakasimama. 31 Na walipokuwa faraghani pamoja wakasema, “Mtu huyu hafanyi jambo lo lote linalostahili kifo au kifungo.” 32 Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kuachiliwa huru kama hakuwa amekata rufaa kesi yake isikilizwe na Kaisari.”