Waefeso 1

1Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu. Kwa watu wa Mungu walio waaminifu kwa Kristo Yesu. 2Nawa takieni neema ya Mungu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 3Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. 4Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. 5Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; 6na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake. 7Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake 8ambayo ametumiminia kwa wingi. 9Kwa maana ametufahamisha kwa hekima yote na ufahamu, siri ya mapenzi yake, kulingana na mpango aliokusudia kuukamilisha kwa njia ya Kristo. 10Mpango huo ambao ungetekelezwa wakati ukitimia, ni kwamba Mungu ataviunganisha vitu vyote po pote vilipo, mbinguni na duniani, viwe kwake chini ya Kristo. 11Tukiwa ndani ya Kristo, tulichaguliwa kama alivy opanga Mungu kwa makusudio yake yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. 12Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake. 13Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa, 14yeye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoupokea, kwa sifa ya utukufu wake. Shukrani Na Maombi

15Hii ndio sababu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana wetu Yesu, na juu ya upendo mlio nao kwa watu wa Mungu, 16sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu. 17Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni roho ya hekima na ya mafunuo mpate kumfahamu zaidi. 18Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. 22Na Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa, 23ambalo ni mwili wake, nalo limejawa na yeye ambaye hujaza kila kitu kwa kila njia. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo