Warumi 1

1Kutoka kwa Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo na mtume niliyecha guliwa na kuitwa kuhubiri Habari Njema ya Mungu. 2Habari hii aliiahidi tangu zamani kwa njia ya manabii wake katika Maandiko matakatifu.

3Habari hii njema ni kuhusu Mwana wa Mungu ambaye kimwili alizaliwa katika ukoo wa Daudi, 4na ambaye alidhihiri shwa kuwa Mwana wa Mungu kwa uwezo wa Roho wa utakatifu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Yeye ndiye Yesu Kristo Bwana wetu, 5ambaye kutoka kwake, na kwa ajili yake, tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii. 6Ninyi pia ni miongoni mwa watu walioitwa kuwa wafuasi wa Yesu Kristo.

7Basi, nawatakieni ninyi nyote mlioko huko Roma, ambao ni wapendwa wa Mungu mlioitwa muwe watakatifu, neema na amani ito kayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Maombi Na Shukrani

8Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. 9Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote ninapo hubiri Habari Njema ya Mwanae, anajua jinsi ninavyowakumbuka siku zote 10katika sala zangu kila ninapoomba. Namwomba Mungu, akipenda, hatimaye sasa nipate nafasi ya kuja kwenu. 11Ninata mani sana kuwaona ili niwagawie zawadi ya kiroho ya kuwaima risha, 12yaani tuimarishane: mimi nitiwe moyo kwa imani yenu na ninyi mtiwe moyo kwa imani yangu.

13Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimeku sudia kuja kwenu, ingawa mpaka sasa nimezuiliwa. Ningependa kupata mavuno ya waamini kati yenu kama nilivyofanikiwa kupata waamini kati ya watu wa mataifa mengine.

14Ninawajibika kwa watu wote, Wagiriki na wasiokuwa Wagi riki; wenye elimu na wasiokuwa na elimu. 15Ndio maana ninata mani sana kuhubiri Injili kwenu ninyi pia mlioko Roma.

16Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia. 17Kwa maana Habari hii Njema inaonyesha wazi haki inayotoka kwa Mungu. Haki hii hupatikana kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Wenye haki wataishi kwa imani.”

Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu

18Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wa wanadamu ambao kwa uovu wao wanauficha ukweli usijulikane. 19Kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao kwa sababu Mungu mwenyewe ameyaweka wazi. 20Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.

21Ingawa walimjua Mungu, hawakumpa heshima na utukufu anaostahili wala kumshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao zilizopumbaa zikatiwa giza. 22Wakijidai kuwa ni werevu, wakawa wajinga. 23Wakauacha utukufu wa Mungu aishiye milele wakageukia sanamu zinazofanana na mwanadamu ambaye hufa, na ndege na wanyama na viumbe vitambaavyo.

24Kwa hiyo, Mungu aliwaacha waendelee kufuata tamaa mbaya za mioyo yao na kutenda matendo ya unajisi nakufanyiana mambo ya aibu katika miili yao. 25Hii ni kwa sababu walikataa ukweli ku husu Mungu wakaamua kuamini uongo; wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba ahimidiwaye milele! Amina.

26Kwa hiyo, Mungu aliwaachia wafuate tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao waliacha matumizi ya asili ya maumbile yao wakatumia miili yao isivyokusudiwa. 27Hali kadhalika wanaume waliacha uhusiano wa asili kati ya waume na wake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume walifanyiana mambo ya aibu, nao waka pata katika miili yao adhabu waliyostahili kama matokeo ya uovu wao.

28Zaidi ya hayo, kwa sababu walikataa kumtambua Mungu, yeye aliwaacha katika nia zao za upotovu watende mambo yasiyosta hili kutendwa. 29Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30wasingiziaji, wanaomchukia Mu ngu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno; wenye hila, wasiotii wazazi wao; 31niwajinga, wasioamini, wasio na huruma nawaka tili. 32Ingawa wanafahamu sheria ya Mungu kwamba watu wanaoishi maisha ya namna hii wanastahili mauti, bado wanaendelea kutenda mambo haya na kuwasifu wengine wafanyao kama wao.