Paulo Anajitetea Mbele Ya Festo
1Siku tatu baada ya Festo kuwasili Kaisaria kuanza kazi, alisafiri kwenda Yerusalemu. 2 Makuhani wakuu na viongozi wa Way ahudi wakamletea mashtaka yao juu ya Paulo, na wakamwomba Festo 3 awafanyie upendeleo, amrudishe Paulo Yerusalemu; wakiwa na mpango wa kumwua Paulo njiani. 4 Festo akawajibu, “Paulo yuko kizuizini huko Kaisaria, na mimi natarajia kwenda huko hivi kari buni. 5 Kwa hiyo tumeni viongozi wenu tuongozane pamoja na kama huyu mtu amefanya kosa lo lote, wao walete mashtaka yao.” 6 Festo alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi kisha akaondoka kwenda Kaisaria. Kesho yake akakaa katika baraza la mahakama, akaamuru Paulo aletwe. 7 Paulo alipoletwa, wale Wayahudi wal iotoka Yerusalemu walisimama wakaanza kutoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha. 8 Lakini Paulo alijitetea, akasema, “Sikufanya jambo lo lote kinyume cha sheria za Wayahudi au Hekalu au kinyume cha Kaisari. ” 9 Festo akitaka kuwapendeza Wayahudi, alimwuliza Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu ukahojiwe huko kuhusu mashtaka haya mbele yangu?” 10 Paulo akasema, “Mimi nasimama mbele ya baraza la mahakama ya Kaisari. Baraza hili ndilo lina wajibu wa kusikiliza kesi hii. Kama unav yojua sijawatendea Wayahudi uovu wo wote. 11 Kama mimi ni mhal ifu na nimetenda kosa linalostahili hukumu ya kifo, sijitetei ili nisiuawe; lakini kama mashtaka yao juu yangu hayana msingi, hakuna mtu atakayeweza kunitia mikononi mwao waniue. Ninakata rufaa, kesi yangu isikilizwe na Kaisari.” 12 Festo akajadiliana na baraza kisha akasema, “Umeomba rufaa usikilizwe na Kaisari; basi utakwenda kwa Kaisari.”
Paulo Afikishwa Mbele Ya Mfalme Agripa
13 Baada ya siku chache mfalme Agripa na Benike wakafika Kaisaria kumkaribisha Festo. 14 Kwa kuwa walikuwa wanakaa Kais aria kwa muda mrefu, Festo alipata nafasi ya kujadiliana na mfalme kesi ya Paulo; akamwambia, “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Feliksi alimwacha gerezani kama mfungwa. 15 Nilipokwenda Yerus alemu, makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka yao juu yake wakitaka ahukumiwe. 16 Lakini mimi niliwaambia kwamba sheria za Kirumi haziruhusu kumhukumu mtu aliyeshitakiwa kabla hajapata nafasi ya kukutana uso kwa uso na washitaki wake naye apewe nafasi ya kujitetea. 17 Walipofika hapa pamoja nami, siku kawia, bali nilikaa pamoja na baraza la mahakama nikaamuru mshta kiwa aletwe. 18 Lakini washtaki wake waliposimama, hawakutaja aina yo yote ya uhalifu kama nilivyotarajia, 19 bali walikuwa na mashtaka kuhusu mabishano fulani juu ya dini yao na juu ya mtu aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo alidai kwamba anaishi. 20 Sikujua jinsi ya kuchunguza mambo haya kwa hiyo nikamwuliza Paulo kama angelipenda kwenda Yerusalemu mashtaka haya yakasiki lizwe huko. 21 Lakini Paulo alipokata rufaa, akaomba akae kizuizini mpaka Kaisari atakapotoa uamuzi wake, niliamuru awekwe rumande mpaka nitakapompeleka kwa Kaisari.” 22 Agripa akasema, “Ningependa nimsikilize mtu huyu mwenyewe.”
Paulo Ajitetea Mbele Ya Agripa
23 Kesho yake Agripa na Bernike walifika kwa fahari kubwa wakaingia katika ukumbi wa mkutano pamoja na mahakimu wa kijeshi na watu mashuhuri wa mji. Ndipo kwa amri ya Festo Paulo akaletwa.
24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, na ninyi nyote mlio hapa pamoja nasi leo, mnamwona hapa huyu mtu ambaye Wayahudi wote wa Yerusalemu na wa hapa Kaisaria wamenisihi, wakipiga makelele kwamba hastahili tena kuishi. 25 Lakini mimi sikuona kosa lo lote alilotenda linalostahili hukumu ya kifo; na kwa kuwa yeye mwenyewe amekata rufaa kesi yake isikilizwe na Kaisari, niliamua nimpeleke kwake. 26 Lakini sina mapendekezo kamili ya kumwandi kia mtukufu Kaisari juu ya huyu mshtakiwa. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu na hasa mbele yako wewe mfalme Agripa ili baada ya kumhoji mshtakiwa nipate jambo la kuandika. 27 Kwa maana ita kuwa si jambo la busara kumpeleka mfungwa kwa Kaisari bila kuon yesha wazi wazi mashtaka yanayomkabili.”