Waamini Wa Efeso Wapokea Roho Mtakatifu
1Wakati Apolo alikuwa Korintho, Paulo alipitia sehemu za kaskazini akafika Efeso. Huko aliwakuta wanafunzi kadhaa, 2aka wauliza, “Mlipoamini mlipokea Roho Mtakatifu?” Wakajibu, “Hapana. Hatujawahi hata kusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 3Ndipo Paulo akawauliza, “Mlibatizwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Ubatizo wa Yohana.” 4Paulo akasema, “Yohana alipobatiza, aliwaambia watu watubu dhambi na kumwamini atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” 5Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Yesu. 6Na Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia , wakasema kwa lugha mpya na kutabiri. 7Walikuwepo kama watu kumi na wawili.
8Paulo akaingia katika sinagogi na kwa muda wa miezi mitatu akafundisha kwa ujasiri akitumia kila njia kueleza juu ya Ufalme wa Mungu. 9Lakini baadhi yao walipokataa kuamini na kuanza kukashifu ujumbe wake mbele ya ushirika wote, aliachana nao, akawachukua wale wanafunzi akaendelea kujadiliana nao katika ukumbi wa Tirano. 10Aliendelea na kazi hii kwa muda wa miaka miwili mpaka wenyeji wote wa Asia wakawa wamesikia neno la Bwana,
Wana Wa Skeva Wajaribu Kutoa Pepo
11Na Mungu alifanya miujiza mingi ya ajabu kwa mkono wa Paulo. 12Watu wakachukua vitambaa na taulo ambazo zilikuwa zimegusa mwili wa Paulo wakawawekea wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao na pepo wachafu wakawatoka. 13Baadhi ya Wayahudi waliokuwa wakienda huku na huko wakiwatoa watu pepo wachafu wali jaribu nao kutumia jina la Yesu kutoa pepo, wakisema, “Nakuamuru kwa jina la Yesu, anayehubiriwa na Paulo.” 14Palikuwa na wana saba wa kuhani mkuu aliyeitwa Skeva ambao walikuwa wakifanya hivi. 15Lakini pepo mchafu akawajibu, “Yesu namfahamu na Paulo pia namfahamu; lakini ninyi ni nani?” 16Yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia akawashambulia vikali, wakatoka ndani ya ile nyumba mbio wakiwa uchi na wenye majeraha. 17Jambo hili likajulikana kwa wenyeji wote wa Efeso, Wayahudi kwa Wagiriki; hofu ikawajaa watu wote; na jina la Bwana likaheshimiwa. 18Waamini wengi wakatubu matendo yao maovu hadharani. 19Na wale waliokuwa wakishiriki uchawi na kupiga ramli wakaleta vitabu vyao na kuvichoma moto hadharani. Walipopiga hesabu ya vitabu walivyochoma walikuta kwamba thamani yake ilikuwa vipande elfu hamsini vya fedha. 20Neno la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.
Ghasia Huko Efeso
21Baada ya mambo haya kutokea, Paulo aliongozwa na Roho kupitia Makedonia na Akaya akiwa njiani kwenda Yerusalemu. Paulo alisema, “Nikishafika Yerusalemu, ni lazima niende Rumi pia.” 22Akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, naye akakaa Asia kwa muda kidogo zaidi. 23Wakati huo huo pakatokea ghasia kubwa kwa sababu ya Njia ya Bwana. 24Mtu mmoja aitwaye Demetrio mhunzi wa vinyago vya fedha alikuwa akitengeneza vihekalu vya fedha vya Artemi na kuwa patia mafundi wake biashara kubwa. 25Yeye aliwakutanisha watu hawa pamoja na watu wengine wanaofanya kazi za kutengeneza viny ago vya miungu kama wao akawaambia, “Jamani, mnajua ya kuwa uta jiri wetu unatokana na kazi zetu. 26Lakini mmeona na kusikia jinsi ambavyo huko Efeso na karibu Asia yote huyu Paulo amewash awishi watu na kutuharibia biashara kwa kusema kuwa miungu iliy otengenezwa na watu si miungu ya kweli. 27Kwa hiyo kuna hatari kuwa kazi yetu itaanza kudharauliwa. Na si hivyo tu, bali hata hekalu la mungu wetu Artemi, aliye mkuu na anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa halina maana tena na utukufu wake utaondolewa.”
28Waliposikia maneno haya walighadhabika wakapiga kelele, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 29Mji mzima ukajaa vurugu, waka kimbilia katika ukumbi wa michezo kwa pamoja wakawakamata Gayo na Aristarko, Wamakedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo. 30Paulo alitaka kuingilia kati lakini wanafunzi wengine wakam zuia; 31hata baadhi ya viongozi waliokuwa marafiki wa Paulo walituma watu wamsihi asiingie katika ule ukumbi. 32Pakawa na kutokuelewana katika ule ukumbi kwa sababu baadhi ya watu wali kuwa wakisema jambo moja na wengine lingine. Ikawa ni fujo; wengi wa watu waliofika hawakujua ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko. 33Wayahudi wakamchagua Aleksanda azungumze kwa niaba yao naye akawaashiria watu wanyamaze apate kuzungumza. 34Lakini umati ulipogundua yakuwa yeye ni Myahudi, walipiga kelele kwa kiasi cha saa mbili wakisema, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 35Baadaye karani wa mji alipofanikiwa kuwanyamazisha, aliwahu tubia akasema, “Ndugu Waefeso, kila mtu ulimwenguni anajua ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu iliyoanguka kutoka angani. 36Kwa hiyo, kwa kuwa hakuna anayeweza kukanusha mambo haya, sioni sababu ya ninyi kufanya fujo au kuchukua hatua ambazo baadaye huenda mkazijutia. 37Kwa maana mmewaleta hawa watu wawili hapa ingawa wao hawaja fanya uharibifu wo wote kwa hekalu la Artemi au kusema maneno ya kufuru juu ya huyu mungu wetu mwanamke. 38Kama Demetrio na mafundi wenzake wana mashtaka juu ya mtu ye yote, mahakama ziko wazi na mahakimu wapo; wachukue hatua za kisheria. 39Lakini kama kuna mashauri mengine, itabidi mtumie baraza halali. 40Hivi sasa tuko katika hatari ya kushtakiwa kwa kufanya fujo kwa maana hatuna sababu ya kuridhisha kuhusu mambo yaliyotokea leo.” 41Baada ya kusema haya akavunja mkutano.