Matendo Ya Mitume 20

Paulo Aenda Makedonia na Ugiriki

1Fujo zilipokwisha, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawa tia moyo halafu akawaaga. Akaanza safari yake ya kwenda Makedo nia. 2Alipokuwa akisafiri, aliwapa waamini katika sehemu zote alizopita maneno ya kuwatia moyo, ndipo akaenda Ugiriki 3ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa akijiandaa kwenda Siria kwa meli, iligundulika kwamba Wayahudi walikuwa na mpango wa kumwua, kwa hiyo akaamua kurudi akipitia Makedonia. 4Watu waliofuatana naye safarini ni Sopatro Piro mwenyeji wa Beroya , Aristako na Sekundo kutoka Thesalonike, Gayo mwenyeji wa Derbe; Timotheo, Tikiko na Trofimo wenyeji wa Asia. 5Hawa walitutangu lia wakaenda kutungojea Troa. 6Sisi tuliondoka baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa hamira tukasafiri kwa meli na kuungana nao siku tano baadaye huko Troa ambako tulikaa kwa siku saba.

Paulo Akutana Na Waamini Wa Troa

7Jioni siku ya kwanza ya Juma tulikuwa tumekutana pamoja kwa chakula na Paulo akaongea nao akiwa na mpango wa kuondoka kesho yake; akaendelea na mazungumzo mpaka usiku wa manane. 8Chumba cha ghorofani walipokuwa wakikutania kilikuwa na taa nyingi 9na kijana mmoja jina lake Eutiko alikuwa amekaa dirishani. Paulo alivyoendelea kuongea kijana huyu alizidi kusinzia. Hatimaye alishikwa na usingizi kabisa, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu, akadhaniwa kuwa amekufa. 10Lakini Paulo alishuka chini akainama, akamkumbatia yule kijana akasema, “Msiwe na hofu, yun gali hai.” 11Paulo akarudi ghorofani na alipokwisha kula, akaongea nao tena mpaka alfajiri ndipo akaondoka. 12Yule kijana alichukuliwa nyumbani akiwa hai na wote waliokuwepo walifarijika.

Paulo Atoka Troa Kwenda Mileto

13Tuliingia katika meli tukasafiri mpaka Aso ambako tuli tarajia kumchukua Paulo kwa maana alikuwa amepanga kusafiri nchi kavu mpaka huko. 14Alipotukuta huko Aso, tulimchukua melini tukasafiri wote mpaka Mitilene. 15Kutoka Mitilene tuliendelea kwa meli na kesho yake tukafika pwani ya upande wa pili wa Kio. Siku iliyofuata tukafika Samo na kesho yake tukawasili Mileto. 16Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi katika jimbo la Asia; kwa sababu alitaka kama ikiwezekana afike Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.

Paulo Anawaaga Wazee Wa Kanisa La Efeso

17Paulo akiwa Mileto, alituma ujumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa wakutane naye. 18Walipofika aliwaambia, “Ninyi mnajua jinsi nilivyoishi nanyi tangu siku ya kwanza nilipofika Asia. 19Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu na machozi na kwa mateso yaliyotokana na njama za Wayahudi. 20Mnajua jinsi ambavyo sikusita kuwaambia cho chote ambacho kingekuwa cha faida kwenu, na jinsi nilivyofundisha hadharani na nyumba kwa nyumba 21nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki juu ya kutubu dhambi kwa Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22Na sasa nimevutwa na Roho niende Yerusalemu na sijui mambo yatakayonipata huko. 23Ila katika kila mji niliopitia, Roho Mtakatifu amenifunulia kwamba mbele yangu kifungo na mateso vinaningoja. 24Lakini nay ahesabu maisha yangu kuwa si kitu cha thamani kwangu, ili mradi niweze kukamilisha wito na kazi niliyopewa na Bwana Yesu; kazi ya kuwashuhudia watu kuhusu Habari Njema ya neema ya Mungu. 25Na sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja wenu, ninyi ambao kati yenu nimekuwa nikihubiri juu ya Ufalme wa Mungu, atakayeniona tena. 26Kwa hiyo nawashuhudia wazi leo hii kwamba sina lawama juu ya mtu ye yote kati yenu, 27kwa sababu sikuacha kuwatangazia mpango kamili wa Mungu. 28Jilindeni nafsi zenu, na mlinde kundi lote la kondoo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka chini ya uongozi wenu; mtunze kanisa la Mungu ambalo amelinunua kwa damu ya Mwa nae. 29Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. 30Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate. 31Kwa hiyo muwe macho; mkumbuke jinsi nilivyomwonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu. 32Na sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake ambalo linaweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi pamoja na wote ambao wameta kaswa. 33Sikutamani fedha au dhahabu au nguo za mtu ye yote. 34Ninyi wenyewe mnajua kwamba kwa mikono yangu nimefanya kazi nikapata mahitaji yangu na ya wenzangu. 35Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii mtaweza kuwa saidia walio dhaifu, mkikumbuka maneno aliyosema Bwana Yesu kwamba, ‘Kuna baraka kubwa zaidi katika kutoa kuliko kupokea.”’

36Paulo alipomaliza kusema haya alipiga magoti akaomba pamoja nao wote. 37Na wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kum busu, 38wakihuzunika kwa sababu ya maneno aliyowaambia kwamba hawatamwona tena. Wakamsindikiza wakamfikisha kwenye meli.