Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu
1Siku moja Petro na Yohana walikwenda Hekaluni saa tisa kwa sala ya adhuhuri. 2Karibu na mlango uitwao Mzuri, palikuwa na mtu aliyekuwa amelemaa tangu kuzaliwa. Kila siku huyo mlemavu aliwekwa karibu na lango la Hekalu akawa akiomba fedha kwa watu waliokuwa wakiingia ndani ya Hekalu. 3Alipowaona Petro na Yohana wakielekea Hekaluni, aliwaomba wampe cho chote. 4Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tuangalie!” 5Akawakodolea macho akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
6Lakini Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu za kukupa, lakini nitakupa kile nilicho nacho. Kwa jina la Yesu wa Nazareti nakuamuru, tembea!” 7Petro akamshika yule mtu mkono, akamwinua, akasimama kwa miguu yake mwenyewe. Mara miguu na viungo vyake vikapata nguvu. 8Akaruka juu, akasimama, akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akirukaruka na kumsifu Mungu. 9Watu wote walimwona akitembea na kumsifu Mungu 10wakam tambua kuwa ni yule mlemavu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango akiomba omba. Wakashangaa mno kuhusu maajabu yaliyomtokea.
Petro Anashuhudia Kuwa Yesu Aponya
11Yule mtu aliyeponywa alipokuwa bado anawang’ang’ania Petro na Yohana, watu wakawakimbilia mpaka kwenye ukumbi wa Sule mani wakiwa wamejawa na mshangao.
12Petro alipoona watu wamekusanyika aliwaambia, “Watu wa Israeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao? Mnadhani ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemwezesha mtu huyu kutembea? 13Sivyo! Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo na wa baba zetu amemtukuza mtumishi wake Yesu kwa muujiza huu. Ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato ijapokuwa Pilato alitaka kufuta mashtaka na kumwachilia. 14Ninyi mlimkataa aliyekuwa Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 15Hivyo mkamwua aliye chanzo cha Uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Sisi ni mashahidi wa mambo haya. 16Imani katika jina la Yesu imempa nguvu huyu mtu ambaye mnamwona na kumfahamu. Ni kwa jina la Yesu na imani inay opatikana kwake ambayo imemponya huyu mtu kabisa, kama ninyi wenyewe mnavyoona.
17“Na sasa ndugu zangu, najua ya kuwa mambo mliyomtendea Yesu, ninyi na viongozi wenu, mliyafanya kwa kutokujua. 18Lakini Mungu alikuwa ametabiri kwa njia ya manabii wake wote kwamba Kristo angeteswa, na hivi ndivyo alivyotimiza utabiri huo. 19Kwa hiyo tubuni mumgeukie Mungu, ili azifute dhambi zenu, 20na mpate nguvu za kiroho kutoka kwa Bwana. Naye atampeleka Kristo, yaani Yesu, ambaye alichaguliwa tangu awali kwa ajili yenu. 21Yeye hana budi kukaa mbinguni mpaka wakati Mungu ataka pofanya kila kitu kuwa kipya tena, kama alivyotamka tangu zamani, kwa kupitia kwa manabii wake watakatifu. 22Kama Musa alivy osema, ‘Bwana Mungu atawateulia nabii kati ya ndugu zenu kama alivyoniteua mimi. Mtamtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. 23Mtu ye yote ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatengwa daima na watu wake na kuangamizwa.’
24“Manabii wote tangu wakati wa Samweli na kuendelea pia walitabiri kuhusu siku hizi. 25Ninyi ni wana wa manabii na wa ile ahadi ambayo Mungu aliwapa baba zenu, alipomwambia Abrahamu, ‘Kutokana na uzao wako familia zote ulimwenguni zitabarikiwa.’ 26Mungu alipomfufua mtumishi wake alimtuma kwenu kwanza ili awaletee baraka kwa kuwawezesha kuacha uovu wenu.”