Paulo Aenda Korintho
1Baada ya haya, Paulo aliondoka Athene akaenda Korintho. 2Huko alimpata Myahudi mmoja jina lake Akila, mzaliwa wa Ponto, ambaye alikuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu mfalme Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona. 3Akakaa nao na kufanya kazi na Akila kwa sababu wote wawili walikuwa mafundi wa kutengeneza mahema. 4Kila siku ya sabato Paulo alikwenda katika sinagogi akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki waamini. 5Sila na Timotheo walipofika kutoka Makedonia walimkuta akihubiri na kuwashuhudia Wayahudi na Wagiriki, kuwa Yesu ndiye Kristo. 6Wal ipombishia na kumtukana alikung’uta mavazi yake akawaambia, “Mimi sina lawama, mkipotea , lawama iko juu yenu wenyewe. Tangu sasa nitawahubiria mataifa neno la Mungu.” 7Kwa hiyo Paulo akaondoka akaenda kwenye nyumba ya mtu anayeitwa Titio Yusto ali yekuwa mcha Mungu. Nyumba yake ilikuwa karibu sana na sinagogi. 8Kiongozi wa hilo sinagogi aliyeitwa Krispo akamwamini Bwana pamoja na jamaa yake; na Wakorintho wengi waliomsikia Paulo wakaamini na kubatizwa. 9Usiku mmoja Bwana akazungumza na Paulo katika ndoto akamwambia, “Usiogope, endelea kuhubiri wala usi kate tamaa. 10Kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia na kukudhuru; kwa kuwa kuna watu wengi walio wangu katika mji huu.” 11Kwa hiyo Paulo akakaa Korintho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, akiwafundisha waamini neno la Mungu. 12Lakini wakati Galio alipofanywa kuwa Liwali wa Akaya, Wayahudi waliungana kumshambulia Paulo, Wakamkamata na kumpeleka Mahakamani. 13Wakamshitaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria zetu.” 14Paulo alipo taka kujitetea Galio akawaambia Wayahudi, “Kama mashtaka yenu yalihusu makosa ambayo mtu huyu amefanya au kama yangehusu ujam bazi, ningewasikiliza. 15Lakini kwa kuwa kesi hii inahusu maneno na majina yaliyo katika sheria zenu, itawabidi muiamue wenyewe. Nakataa kabisa kujihusisha na jambo hili.” 16Akawafu kuza kutoka mahakamani. 17Wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya mahakama. Wala Galio hakuingilia kati.
Paulo Arudi Antiokia
18Baada ya haya Paulo alikaa huko Korintho kwa siku nyingi zaidi kisha akaagana na wale ndugu waamini akasafiri kwa meli kuelekea Siria akiongozana na Prisila na Akila. Walipofika Kenk rea Paulo alinyoa nywele zake kwa maana alikuwa ameweka nadhiri. 19Walipofika Efeso Paulo aliwaacha Prisila na Akila, akaenda katika sinagogi akawa akijadiliana na Wayahudi. 20Walipomwambia akae nao kwa muda mrefu zaidi alikataa, 21lakini alipokuwa aki waaga aliwaambia, “Nitarudi kama Mungu akipenda.” Akasafiri kwa meli kutoka Efeso. 22Alipofika Kaisaria alikwenda kuwasalimu ndugu katika kanisa kisha akaelekea Antiokia. 23Alikaa Antiokia kwa muda, na baadaye aliondoka akatembelea makanisa huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha waamini wote.
Apolo Ahubiri Efeso Na Korintho
24Basi Myahudi mmoja jina lake Apolo, mwenyeji wa Aleksan dria alikuja Efeso. Yeye alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhu biri na pia aliyajua Maandiko barabara. 25Alikuwa amefundishwa njia ya Bwana naye akiwa amejaa moto wa kiroho alifundisha kwa usahihi juu ya Yesu. Lakini ujuzi wake uliishia kwenye ubatizo wa Yohana. 26Apolo alihubiri kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.