Luka 8

1Baada ya haya Yesu alikwenda katika miji na vijiji akifu atana na wanafunzi wake. Kila alipokwenda alihubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu.

2Baadhi ya wanawake aliokuwa amewatoa pepo wachafu na kuwa ponya walifuatana naye. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu ambaye aliitwa Magdalena, aliyetolewa pepo saba; Yohana mke wa Chuza -msimamizi wa ikulu ya Herode; Susana, na wengine wengi. Wana wake hawa walimhudumia Yesu na wanafunzi wake kutokana na mapato yao wenyewe.

4Watu wengi walimiminika kutoka katika kila mji na umati mkubwa ulipokusanyika, Yesu akawaambia mfano huu: 5“Mkulima mmoja alikwenda shambani kwake kupanda mbegu. Alipokuwa akitawa nya mbegu, nyingine zilianguka njiani zikakanyagwa kanyagwa; na ndege wakazila. 6Na mbegu nyingine zilianguka penye miamba na zilipomea zikakauka kwa kukosa unyevu. 7Na mbegu nyingine zil ianguka kwenye miiba, ikazisonga zikafa. 8Mbegu nyingine zilian guka penye udongo mzuri, nazo zikamea na kutoa mazao mara mia zaidi ya mbegu alizopanda.” Baada ya kutoa mfano huu akasema: “Mwenye nia ya kusikia na asikie!”

9Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano huu. 10Naye akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waan galie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’ 11Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. 12Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa. 13Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

Mfano Wa Taa

16“Ni nani anayewasha taa kisha akaifunika, au akaiweka uvunguni, badala ya kuiweka mahali ambapo mwanga wake utaonekana? 17Hakuna siri ambayo haitafichuliwa, wala hakuna jambo lililo fichika ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi. 18Kwa hiyo muwe waangalifu mnaposikiliza, kwa sababu, yeye aliye na kitu ataonge zewa, naye ambaye hana, atanyang’anywa hata kile anachodhania anacho.”

Ndugu Wa Kweli

19Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kum wona lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. 20Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” 21Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

Bwana Yesu Atuliza Dhoruba

22Siku moja Yesu alipanda mashua na wanafunzi wake akawaam bia, “Twendeni ng’ambo ya pili ya ziwa.” Kwa hiyo wakaanza kuvuka. 3Walipokuwa wakivuka, akalala usingizi. Upepo mkali ukawa unavuma na mashua yao ikaanza kujaa maji; wakawa katika hatari ya kuzama.

24Wale wanafunzi wakamkimbilia Yesu wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana, tunazama!” Ndipo akaamka akaukemea ule upepo na yale mawimbi vikakoma, pakawa shwari. 25Kisha akawauliza, “Imani yenu iko wapi?” Wakashangaa na kuogopa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu ambaye anaamuru upepo na mawimbi navyo vikamtii?”

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo

26Basi wakawasili ng’ambo ya pili katika jimbo la Wagerasi. 27Na aliposhuka katika mashua alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyepagawa na pepo. Kwa muda mrefu mtu huyu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. 28Alipomwona Yesu alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kuu, “Unataka nini kwangu, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu?

Nakuomba, tafadhali usinitese!”

29Wakati huo Yesu alikuwa ameanza kumwamuru yule pepo mchafu amtoke. Mara nyingi pepo huyo alimwingia na hata alipo fungwa na minyororo na kuwekwa chini ya ulinzi aliivunjilia mbali minyororo hiyo na kukimbilia jangwani akiwa ametawaliwa kabisa na pepo huyo. 30Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jeshi’ 31Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda shimoni kwenye kifungo cha mashetani.

32Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo karibu wakilisha kando kando ya mlima. Wale pepo wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe. Akawaruhusu.

33Kwa hiyo wakamtoka yule mtu wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe likatimka mbio katika ule mteremko mkali wakatumbukia ziwani na kuzama. 34Watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe waliona yaliyotokea, wakakimbia wakaeneza habari hizi mjini na mashambani.

35Watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotokea. Wali pofika hapo alipokuwa Yesu wakamwona yule mtu aliyetokwa na pepo amekaa karibu na Yesu, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa sana. 36Wale walioona mambo yalivyotokea wakawasimu lia wenzao jinsi yule mtu alivyoponywa. 37Watu wote wa jimbo hilo la Wagerasi wakamwomba Yesu aondoke kwao, kwa sababu wali kuwa wamejawa na woga. Basi akaingia katika mtumbwi akaondoka.

38Yule mtu aliyetolewa pepo akamsihi Yesu afuatane naye. Lakini Yesu akakataa, akamwambia: 39“Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu aliyokufanyia Mungu.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza mji mzima mambo makuu Yesu aliyomfanyia.

Yesu Amfufua Binti Wa Yairo

40Yesu aliporudi ng’ambo ya pili umati mkubwa wa watu ukam pokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea.

41Wakati huo akaja mtu mmoja jina lake Yairo, kiongozi wa sinagogi. Akapiga magoti mbele ya Yesu akamwomba afike nyumbani kwake, 42kwa kuwa binti yake mwenye umri wa miaka kumi na mbili, aliyekuwa mtoto wake wa pekee, alikuwa mgonjwa mahututi, karibu ya kufa. Yesu alipokuwa akienda, umati ulimsonga sana.

43Katika umati huo alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, wala hakuna mganga aliyeweza kumponya. 44Akaja nyuma ya Yesu, akam gusa pindo la vazi lake. Mara damu iliyokuwa ikimtoka ikakauka, akapona. 45Yesu akauliza: “Nani amenigusa?” Kila mtu alipo kana Petro akasema, “Bwana, watu ni wengi mno wanaokusonga kila upande.” 46Yesu akasema: “Kuna mtu aliyenigusa maana naona ya kuwa nguvu za kuponya zimenitoka.” 47Yule mama alipofahamu ya kuwa amegundulika akaja huku akitetemeka akapiga magoti mbele ya Yesu. Akamweleza Yesu mbele ya watu wote kilichomfanya amguse, na jinsi alivyoponywa mara. 48Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” 49Wakati Yesu alipo kuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo kum wambia, “Binti yako amefariki. Hakuna sababu ya kuendelea kum sumbua Mwalimu.” 50Lakini Yesu aliposikia haya alimwambia Yairo, “Usiogope. Uwe na imani na binti yako atapona.” 51Wal ipofika kwa Yairo akawazuia watu wote wasiingie ndani isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, na baba na mama wa yule binti. 52Watu waliokuwepo walikuwa wakilia na kuomboleza lakini Yesu akawaam bia, “Acheni kulia! Huyu binti hajafa ila amelala!” 53Wao wakamcheka kwa dharau maana walijua amekwisha kufa. 54Yesu akamshika yule binti mkono akamwita: “Binti, amka!” 55Uhai ukamrudia, naye akasimama mara moja. Yesu akaamuru apewe chakula. 56Wazazi wake wakastaajabu sana lakini Yesu akawakataza wasim wambie mtu alivyomfufua binti yao.