Luka 11

1Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” 2Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. 3Utupatie chakula chetu kila siku. 4Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” 5Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ 7Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ 8“Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. 9Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11“Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12Au akimwomba yai atampa nge? 13Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho

Yesu Na Beelzebuli

14Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23“Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.

24“Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”

27Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”

Ishara Ya Yona

29Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 30Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa. 31Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa. 32Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko

Taa Ya Mwili

33“Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”

Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria

37Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja. 38Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa. 39Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.

42“Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.

43“Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni! 44Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

45Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!” 46Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza. 47Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu. 48Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.

49“Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’ 50Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki; 51tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote. 52Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”

53Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi, 54wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.