1Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ili kuwa imekaribia. 2Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu kwa siri kwa sababu waliwaogopa watu.
3Shetani akamwingia Yuda aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili. 4Yuda akaenda kwa makuhani wakuu na wakubwa wa walinzi wa Hekalu akawaeleza jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 5Wakafurahi na wakaahidi kumlipa fedha. 6Naye akaridhika, akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti Yesu kwa siri. Maandalizi Ya Chakula Cha Pasaka
7Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.” 9Wakam wuliza, “Tukaandae wapi?” 10Akawajibu, “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia, 11kisha mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? 12Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani ambacho kina fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.”
13Wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaam bia. Kwa hiyo wakaandaa chakula cha Pasaka.
14Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15Kisha akawaambia “Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, “Chukueni mnywe wote. 18Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. 21Lakini huyo atakayenisaliti amekaa nasi hapa mezani kama rafiki. 22Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivyokusudiwa na Mungu, lakini ole wake huyo mtu atakayenisaliti.” 23Wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao angefanya kitu kama hicho.
Ubishi Kuhusu Ukubwa
24Pia ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa kati yao. 25Yesu akawaambia, “Wafalme wa dunia huwatawala watu wao kwa mabavu na wenye mam laka huitwa ‘Wafadhili.’ 26Ninyi msifanye hivyo. Aliye mkubwa wenu awe kama ndiye mdogo kabisa; na kiongozi wenu awe kama mtum ishi. 27Kwani mkubwa ni nani? Yule aketiye mezani au yule anayemhudumia? Bila shaka ni yule aliyekaa mezani. Lakini mimi niko pamoja nanyi kama mtumishi wenu.
28“Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu: 29na kama Baba yangu alivyonipa mamlaka ya kutawala; mimi nami nina wapa ninyi mamlaka hayo hayo. 30Mtakula na kunywa katika karamu ya Ufalme wangu na kukaa katika viti vya enzi mkitawala makabila kumi na mawili ya Israeli.”
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
31Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, shetani ameomba ruhusa kwa Mungu awapepete ninyi kama ngano. 32Lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipotee. Na utakaponirudia mimi, uwatie moyo ndugu zako.”
33Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”
Kujiandaa Wakati Wa Hatari
35Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga. 37Kwa sababu, nawambieni, yale Maandiko yaliyosema kwamba ‘Alihesabiwa pamoja na wahalifu’ yananihusu mimi na hayana budi kutimizwa. Naam, yale yaliyoandikwa kunihusu mimi yanatimia.” 38Wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna mapanga mawili.” Akawajibu, “Inatosha!. Yesu Asali Kwenye Mlima Wa Mizeituni
39Ndipo Yesu akaondoka kuelekea kwenye mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, na wanafunzi wake wakamfuata. 40Alipofika huko akawaambia wanafunzi, “Ombeni kwamba msiingie katika majaribu.” 41Akaenda mbali kidogo nao, kama umbali anaoweza mtu kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kwa mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike.” [ 43Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni. 46Akawauliza, “Mbona mnalala? Amkeni muombe ili msiingie katika majaribu.”
Yesu Akamatwa
47Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu. 48Lakini Yesu akamwuliza, “Yuda! Unanisaliti mimi Mwana wa Adamu kwa busu?” 49Wafuasi wa Yesu walipoona yanayotokea, wakasema, “Bwana, tutumie mapanga yetu?” 50Na mmoja wao akampiga mtum ishi wa kuhani mkuu kwa panga, akamkata sikio la kulia. 51Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa sikio la yule mtu, akamponya. 52Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”
Petro Amkana Yesu
54Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa
63Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
66Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.” 70Wote wakasema, “Ndio kusema wewe ndiye Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Ninyi ndio mmesema kwamba Mimi ndiye.” 71Kisha wakasema, “Kwa nini tutafute ushahidi zaidi? Sisi wenyewe tumesikia maneno aliy osema.” Yesu Apelekwa Kwa Pilato