Yesu Awaonya Na Kuwafariji Wanafunzi
1Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.
2“Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4“Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi. 5Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! 6Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. 7Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 8“Ninawaambia, kila atakayenikiri mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkiri mbele ya malaika wa Mungu. 9Lakini kila anayenikana mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkana mbele ya malaika wa Mungu. 10Na kila atakayesema neno baya kunihusu mimi Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11“Na watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
13Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14Yesu akamwam bia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mga wanyaji wa urithi wenu?” 15Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”
16Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19Na nitasema moy oni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21Hivi ndivyo itakavy okuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”
22Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo! 28Ikiwa Mungu huyav isha hivi majani ambayo leo yapo shambani na kesho yanachomwa moto; ataachaje kuwavisha ninyi hata zaidi? Mbona mna imani ndogo! 29Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 30Watu wasiomjua Mungu huhan gaika sana juu ya vitu hivi. Lakini Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji. 31Basi, tafuteni Ufalme wa Mungu; na hivyo vyote atawapatia.”
32“Ninyi kundi dogo, msiogope kwa maana Mungu amependa mtawale naye katika ufalme wake. 33Uzeni mali zenu muwape mas kini; ili mjipatie mikoba isiyochakaa, na kujiwekea hazina mbin guni ambapo mwizi hafiki wala nondo haharibu. 34Kwa maana unapoiweka akiba yako ndipo na moyo wako utakapokuwa.”
Kukesha
35“Muwe tayari mkiwa mmevaa, na taa zenu zikiwaka. 36Muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka haru sini, ili atakapokuja na kugonga mlango wamfungulie mara moja. 37Itakuwa ni heri kwa wale watumishi ambao bwana wao akija ata wakuta wanamngoja. Nawaambieni kweli, atajiandaa na kuwaketisha karamuni awahudumie. 38Itakuwa ni furaha kubwa kwao ikiwa ata wakuta tayari hata kama atakuja usiku wa manane au alfajiri.
39Fahamuni kwamba kama mwenye nyumba angalijua ni saa ngapi mwizi atakuja, angalijiandaa asiiachie nyumba yake ivunjwe. 40Kwa hiyo, ninyi pia mkae tayari, kwa maana mimi Mwana wa Adamu nita kuja saa ambayo hamnitegemei.”
Mtumishi Mwaminifu Na Asiye mwaminifu
41Ndipo Petro akamwambia, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” 42Yesu akamwambia, “Ni yupi wakili mwaminifu na mwenye busara? Ni yule ambaye bwana wake atamfanya mtawala juu ya nyumba yake yote naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa. 43Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44Ninawahakikishia kwamba atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. 45Lakini kwa mfano, kama yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi,’ halafu aanze kuwa piga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, 46bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii. 47Na mtumishi ambaye anafahamu mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, pia ataad hibiwa vikali. 48Lakini mtumishi ambaye hafahamu anachotakiwa kufanya na akafanya kitu kinachostahili adhabu, atapata adhabu ndogo. Mungu atatarajia vingi kutoka kwa mtu aliyepewa vipawa vingi; na mtu aliyekabidhiwa vingi zaidi, atadaiwa zaidi pia.”
49“Nimekuja kuleta moto duniani! Laiti kama dunia inge kuwa tayari imeshawaka! 50Lakini kuna ubatizo ambao lazima niu pokee na dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo utakapokamilika.
51“Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambieni sivyo; nimekuja kuleta mafarakano. 52Kuanzia sasa, katika nyumba ya watu watano kutakuwa na mgawanyiko: watatu wakipingana na wawili, na wawili wakipingana na watatu. 53Baba atapingana na mwanae na mwana atapingana na babaye; mama atapingana na bin tiye na binti atapingana na mamaye; mama mkwe atapingana na mke wa mwanae ambaye naye atapingana na mama mkwe wake.”
Kutambua majira
54Kisha Yesu akawaambia watu, “Mkiona wingu likitokea mag haribi, mara moja mnasema, ‘Mvua hiyo inakuja!’ na inakuwa hivyo. 55Na mnapouona upepo wa kusi ukivuma, mnasema, ‘Kutakuwa na joto!’ Na linakuwepo. 56Enyi wanafiki! Mnaweza kutambua dalili za hali ya hewa; kwa nini basi hamtambui maana ya mambo yanayoto kea sasa? 57Kwa nini hamuamui lililo haki kutenda? 58Kama mtu akikushtaki mahakamani, jitahidi sana kupatana na mshtaki wako wakati mkiwa mnaenda mahakamani, ili asikufikishe mbele ya hakimu, na hakimu akakukabidhi kwa polisi, na polisi wakakutia gerezani. 59Nakuhakikishia kwamba, hutatoka huko gerezani mpaka umelipa faini yote.”