1Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao. 5Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu? 6Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.” 8Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote. 10Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao. 11Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili
13Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16lakini wao hawakumtambua. 17Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni. 18Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 20Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha. 21Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri 23lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 24Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?” 27Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari. 29Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” 33Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu? 39Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa, 43akakichukua akakila mbele yao.
44Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” 45Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi. 48Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu; lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu kutoka mbinguni.”
Yesu Apaa Mbinguni
50Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake, akawabariki. 51Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. 52Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;