1Baada ya hayo, Yesu akawachagua wafuasi wengine sabini na wawili akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda. 2Akawaambia, “Mavuno ni mengi lakini wafanya kazi ni wachache, kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno awapeleke wavunaji zaidi katika shamba lake. 3Haya, nendeni. Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. 4Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu; na msipoteze muda kumsalimu mtu ye yote njiani. 5Mkiingia nyumba yo yote kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 6Kama aishiye humo ni mwenye kupenda amani basi baraka hiyo itakaa naye, la sivyo, itawarudia. 7Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa kile watakachowapa kwa sababu kila mfany akazi anastahili kulipwa mshahara. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. 8Mkienda katika mji mkapokelewa: kuleni mtakachoandal iwa; 9waponyeni wagonjwa na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu.’
10“Lakini mkiingia katika mji msikaribishwe, nendeni katika mitaa yake mkaseme: 11‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12“Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto. 14Lakini siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko kwenu. 15Na ninyi je, watu wa Kapernaumu, mnafikiri mtainuliwa juu hadi mbinguni? La, Mungu atawatupa chini hadi kuzimuni. 16“Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.”
17Wale wanafunzi sabini na wawili wakarudi wakiwa na furaha. Wakamwambia Yesu, “Bwana, tukilitumia jina lako, hata pepo wanatutii!” 18Akawajibu, “Nimemwona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni. 19Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru. 20Lakini msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, ila furahini kwa kuwa majina yenu yamean dikwa mbinguni.”
21Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba. 22Baba yangu amenika bidhi mambo yote. Hakuna anayemfahamu Mwana isipokuwa Baba: na hakuna anayemfahamu Baba isipokuwa Mwana na wale ambao Mwana ame penda humdhihirisha Baba kwao.” 23Basi Yesu akawageukia wana funzi wake akawaambia faraghani, “Mmebarikiwa kuona mambo haya mnayoyaona! 24Nawaambie ni kweli, manabii wengi na wafalme wal itamani kuona mnayoyaona na kusikia mnayoyasikia lakini hawaku pata nafasi hiyo.” Mfano Wa Msamaria Mwema
25Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.
33“Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.
36“Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”
37Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38Wakati Yesu na Wanafunzi wake walipokuwa wakiendelea na safari yao ya kwenda Yerusalemu, walifika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha Yesu nyum bani kwake. 39Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Mariamu ambaye aliketi chini karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote. Kwa hiyo alikuja kwa Yesu akalalamika, “Bwana, hujali kwamba mdogo wangu ameniachia kazi zote? Mwambie aje anisaidie!” 41Bwana akamjibu, “Martha! Martha! Mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42Unahitaji kujua kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kil icho bora, na hakuna mtu atakayemnyang’anya.” Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake Kuomba