Luka 23

1Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” 3Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.” 4Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!” 5Lakini wao wakakazana kusema, “Anawa chochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote. Alianzia huko

Yesu Apelekwa Kwa Herode

6Pilato aliposikia hayo akauliza, ‘Huyu mtu ni Mgalilaya?” 7Alipofahamu kwamba Yesu alitoka katika mkoa unaotawaliwa na Herode, akampeleka kwa Herode ambaye wakati huo alikuwa Yerus alemu. 8Herode alifurahi sana kumwona Yesu. Alikuwa amesikia habari zake na kwa muda mrefu akatamani sana kumwona; na pia alitegemea kumwona Yesu akifanya mwujiza. 9Kwa hiyo akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini yeye hakumjibu neno. 10Wakati huo, makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11Herode na maaskari wake wakamkashifu Yesu na kumzomea. Wakamvika vazi la kifahari, wakamrudisha kwa Pilato. 12Siku hiyo, Herode na Pilato, ambao kabla ya hapo walikuwa maadui, wakawa marafiki.

Yesu Ahukumiwa Kifo

13Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu 14aka waambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwa potosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia kutokana na mashtaka mliyoleta. 15Hata Herode hakumwona na kosa lo lote; ndio sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo. 16Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko, kisha nimwachilie.” [ 17Kwa kawaida, kila sikukuu ya Pasaka ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja].

18Watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “ Auawe huyo! Tufungulie Baraba!” 19Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini. 20Pilato ali taka sana kumwachilia Yesu kwa hiyo akasema nao tena. 21Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” 22Kwa mara ya tatu Pilato akasema nao tena, “Amefanya kosa gani huyu mtu? Sioni sababu yo yote ya kutosha kumhukumu adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko kisha nimwachilie .”

23Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu na kusisi tiza kwamba Yesu asulubiwe. Hatimaye, kelele zao zikashinda. 24Pilato akaamua kutoa hukumu waliyoitaka. 25Akamwachia huru yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini; akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfa nyie watakavyo. Yesu Asulubiwa Msalabani

26Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu. 27Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”

32Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu. 33Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.

34Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”

38Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”

40Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”

Yesu Afa Msalabani

44Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

47Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.

49Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini

50Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika. 51Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu. 52Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado. 54Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.