Luka 21

1Alipokuwa Hekaluni Yesu aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la sadaka. 2Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. 3Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. 4Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”

Dalili Za Siku Za Mwisho

5Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuhusu Hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na mapambo maridadi yaliyotolewa kama sadaka kwa Mungu. Yesu akawaambia, 6“Wakati unakuja ambapo vyote hivyo mnavyovistaajabia sasa vitabomolewa, halitabaki hata jiwe moja juu ya jingine.” 7Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakari bia?” 8Akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja wakitumia jina langu, na kusema, ‘Mimi ndiye’ na ‘Wakati umekaribia’. Msiwafuate. 9Na mtakaposikia habari za vita na machafuko, msiogope, kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila mwisho hautatokea wakati huo.”

10Kisha akawaambia: “Taifa moja litapigana na taifa lin gine na utawala mmoja utapigana na utawala mwingine. 11Kutaku wepo na matetemeko ya ardhi, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali; kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.”

Mateso

12“Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13Na hii itawapa nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu imani yenu. 14Lakini msiwe na wasiwasi juu ya matayarisho ya utetezi wenu kabla ya mashtaka. 15Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo maadui zenu hawa taweza kukataa au kupinga. 16Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu mtauawa. 17Watu wote watawa chukia kwa ajili yangu. 18Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! 19Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.”

Kuteketezwa Kwa Yerusalemu

20“Mkiona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, faham uni kwamba karibu utaangamizwa. 21Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani; walio mjini Yerusalemu waondoke humo na wale walioko mashambani wasije mjini. 22Kwa sababu huu utakuwa wakati wa kulipiza kisasi ili yale yote yaliyosemwa kwenye Maan diko yatimie.

23“Ole wao akina mama watakaokuwa waja wazito na wata kaokuwa wakinyonyesha! Kutakuwa na dhiki nchini na ghadhabu ya Mungu itakuwa juu ya watu wa taifa hili. 24Wengine watauawa kwa silaha na wengine watachukuliwa mateka na kupelekwa nchi mbalim bali. Na Yerusalemu itamilikiwa na watu wa mataifa mengine mpaka muda wa mataifa hayo utakapokwisha.”

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

25“Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. 28Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”

29Akawaambia mfano, “Utazameni mtini na miti mingine yote. 30Inapochipua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu. 31Hali kadhalika, mkiyaona mambo haya yanatokea, faham uni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitakwisha kabla mambo haya hayajatokea. 33Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.” Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla

34Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”

37Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni na jioni ili pofika alikwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. 38Na asubuhi na mapema watu wote walikuwa wakija Hekaluni kumsikiliza.