Yesu Apelekwa Kwa Pilato
1Asubuhi na mapema, makuhani wakuu wote na wazee walifanya mkutano, wakashauriana jinsi ya kumwua. 2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato ambaye alikuwa gavana.
Majuto Ya Yuda
3 Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehuku miwa alijuta. Akazirudisha zile fedha alizopewa kwa makuhani wakuu na wazee 4 akawaambia, “Nimetenda dhambi kwa maana nimem saliti mtu asiye na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
5 Basi Yuda akazitupa zile fedha Hekaluni, akaondoka; akaenda akajinyonga.
6 Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” 7 Kwa hiyo baada ya kujadiliana waliamua kuzitumia kununua shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 8 Kwa hiyo shamba hili limeitwa ‘Shamba la damu’ hadi leo. 9 Ndipo yakatimia yale aliyonena nabii Yeremia kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na wana wa Israeli, 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”
Yesu Mbele Ya Pilato
11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.” 12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipomshtaki kwa mambo mengi hakujibu neno. 13 Ndipo Pilato akamwuliza, “Husikii mambo hayo yote wanayokushtaki nayo?” 14 Lakini Yesu hakujibu neno hata kwa shtaka moja. Gavana akashangaa sana.
15 Kila wakati wa sikukuu, gavana alikuwa na desturi ya kum fungua mfungwa mmoja atakayechaguliwa na watu. 16 Wakati huo alikuwapo mfungwa mmoja mwenye kujulikana sana, aliyeitwa Baraba. 17 Basi watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwa fungulie nani; Baraba au Yesu aitwaye Kristo?” 18 Kwa sababu alijua kuwa Yesu aliletwa kwake kwa ajili ya wivu wa viongozi wa Wayahudi. 19 Alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mke wake alimpelekea ujumbe, “Usijihusishe katika kesi ya huyu mtu asiye na hatia. Leo nimehangaika sana katika ndoto kwa ajili yake.”
20 Basi makuhani na wazee wakawashawishi umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe. 21 Gavana akawau liza tena , “Ni yupi mnataka niwafungulie?” Wakajibu, “Bar aba!” 22 “Sasa nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote , “Asulubiwe!” 23 Akasema, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Asulubiwe.”
24 Pilato alipoona kwamba hakuna zaidi ambalo angeweza kufa nya na kwamba ghasia ilikuwa ikianza, akachukua maji, akanawa mikono mbele yao, akasema, “Sina hatia na damu ya mtu huyu. Jambo hili ni juu yenu.”
Jambo hili ni juu yenu.”
25 Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
26 Basi akawafungulia Baraba, na baada ya kuamuru Yesu apigwe viboko, akamtoa asulubiwe.
Askari Wamdhihaki Yesu
27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu. 29 Wakasokota taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.
Yesu Asulubishwa
32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja, akaikataa.
35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia kura. 36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.’ 38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.
39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke kutoka msalabani nasi tutamwamini. 43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa njia hiyo hiyo.
Kifo Cha Yesu
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho. 51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi. 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika, huyu alikuwa
Mwana wa Mungu!”
55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea. 56 Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.
Yesu Azikwa Kaburini
57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.
Walinzi Wa Kaburi
62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.