Yesu Afufuka
1Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. 2Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. 3Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
5Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. 7Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.” 8Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi habari hizo.
9Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam wabudu. 10Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”
Taarifa Ya Askari
11Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea. 12Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.” 15Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake
16Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya kwe nye ule mlima ambao Yesu aliwaagiza. 17Walipomwona, walimwabu du. Lakini baadhi yao waliona mashaka.
18Yesu akawakaribia akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.