Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo
1Kisha Yesu akawaambia ule umati wa watu pamoja na wana funzi wake: 2 “Walimu wa sheria na Mafarisayo wamechukua nafasi ya Musa, 3 kwa hiyo watiini na kufanya yote wanayowaambia mfa nye. Lakini msifuate matendo yao; kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuwabebesha watu, lakini wao wenyewe hawajaribu hata kunyoosha kidole kuisogeza!
5 “Wao hufanya mambo yao yote ili waonekane na watu. Wanavaa vipande vipana vya ngozi vilivyoandikwa sheria na kurefusha zaidi pindo za mavazi yao ya sala. 6 Wanapenda kukaa viti vya wageni wa heshima karamuni na viti vya mbele katika masinagogi. 7 Hupenda kuamkiwa masokoni na kuitwa ‘Rabi.’
8 “Lakini ninyi msipende kuitwa ‘Rabi’ kwa sababu mnaye rabi mmoja, na ninyi nyote ni ndugu. 9 Na msimwite mtu ye yote hapa duniani ‘baba’ kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni. 10 Hali kadhalika msipende kuitwa ‘mabwana’ kwa maana mnaye Bwana mmoja tu, yaani Kristo. 11 Aliye mkuu kuliko ninyi nyote atakuwa mtumishi wenu. 12 Ye yote anayejikuza atashushwa; na ye yote anayejinyenyekeza atainuliwa.
13 “Lakini ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnafungia watu milango ya Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, wala hamruhusu wale ambao wange penda kuingia waingie. [
14 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnadhulumu nyumba za wajane, na kwa kujionyesha kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.”]
15 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja awe mfuasi wa dini yenu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya astahili kwenda Jehena mara mbili zaidi yenu!
16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mnasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu iliyoko Hekaluni, itambidi atimize kiapo hicho.’ 17 Ninyi vipofu wajinga! Ni kipi kilicho bora zaidi, ni ile dhahabu au ni Hekalu ambalo ndilo linafanya dhahabu hiyo kuwa takatifu? 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyoko madhabahuni itambidi atimize kiapo hicho.’ 19 Ninyi vipofu! Ni kipi bora zaidi, sadaka, au madhabahu ambayo ndio inafanya sadaka hiyo kuwa takatifu? 20 Kwa hiyo mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hiyo madhabahu na vitu vyote vilivyoko juu yake. 21 Na mtu anapoapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na huyo aishie ndani yake. 22 Naye anayeapa kwa mbingu anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.
23 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnatoa fungu la kumi la mnanaa, na bizari na jira; lakini mmepuuza mambo makuu zaidi ya sheria: haki, huruma na imani. Haya mlipaswa kuyafanya bila kusahau yale mengine. 24 Ninyi viongozi vipofu, mnachuja nzi lakini mnameza ngamia!
25 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa ulafi na unyang’anyi. 26 Ninyi Mafarisayo vipofu! Kwanza safisheni kikombe na sahani kwa ndani, ndipo nje patakuwa safi.
27 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28 Hali kadhalika, nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
29 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kupamba makaburi ya wenye haki 30 mkisema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu tusingel ishiriki katika kuwaua manabii !’ 31 Kwa kusema hivyo mnakiri kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32 Haya basi, kamilisheni hiyo kazi waliyoianza baba zenu! 33 Ninyi nyoka, ninyi kundi la nyoka! Mtaepukaje hukumu ya Jehena? 34 Kwa sababu hiyo nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwatundika msalabani, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawatesa toka mji mmoja hadi mji mwingine. 35 Na kwa hiyo damu ya wote wenye haki ambayo imemwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia ambaye mlimwua kati kati ya Patakatifu na madhabahu, itakuwa juu yenu. 36 Nawaambia kweli haya yote yatatokea wakati wa kizazi hiki.”
Yesu Awaonya Watu Wa Yerusalemu
37 “Ninyi watu wa Yerusalemu; mnawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Nilitamani sana kuwakusanya wana wenu kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! 38 Tazama nyumba yenu imeachwa tupu na ukiwa. 39 Kwa maana nawahakikishia kuwa, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema: ‘Amebarikiwa yeye anayekuja kwa jina la Bwana.