Mpango Wa Kumwua Yesu
1Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, 2“Mnafahamu kwamba sikukuu ya Pasaka inaanza baada ya siku mbili na mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kusulubiwa.”
3Wakati huo makuhani wakuu na wazee walifanya mkutano katika ukumbi wa kuhani mkuu, jina lake, Kayafa. 4Wakashauriana jinsi ya kumkamata Yesu na kumwua kwa siri. 5Wakasema, “Lakini tusi fanye haya wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
Yesu Anapakwa Mafuta Bethania
6Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, 7mwa namke mmoja alimjia akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya thamani kubwa; akammiminia Yesu manukato hayo kichwani akiwa ame kaa mezani. 8Lakini wanafunzi wake walipoona hayo waliudhika, wakasema, “Kwa nini kupoteza manukato bure? 9Haya yangaliuzwa kwa bei kubwa na fedha hizo wakapewa maskini.”
10Yesu alifahamu mawazo yao kwa hiyo akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Amenifanyia jambo zuri sana. 11Maskini mnao siku zote lakini hamtakuwa nami siku zote. 12Aliponimimi nia haya manukato alikuwa akiandaa mwili wangu kwa mazishi. 13Ninawaambia kweli, mahali po pote Habari Njema itakapohubi riwa ulimwenguni, jambo hili alilofanya litatajwa, kwa ukumbusho wake.”
Yuda Akubali Kumsaliti Yesu
14Kisha mmojawapo wa wale wanafunzi kumi na wawili aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa kuhani mkuu akamwambia, “Mtanilipa kiasi gani nikimtoa kwenu?” 15Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.
Matayarisho Ya Pasaka
17Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza, “Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
18Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, ‘Bwana anasema hivi: saa yangu imekaribia, napenda kula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu nyumbani kwako.’ ” 19Wanafunzi waka fanya kama Yesu alivyowaambia, wakaandaa Pasaka.
20Ilipofika jioni, Yesu aliketi mezani pamoja na wanafunzi wake. 21Walipokuwa wakila akawaambia, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.” 22Wakasikitika sana, wakaanza kumwul iza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 23Yesu akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami, ndiye ata kayenisaliti. 24Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivy oandikwa katika Maandiko, lakini ole wake mtu yule atakayenisal iti. Ingalikuwa nafuu kwake kama hakuzaliwa!”
25Kisha Yuda, yule ambaye alimsaliti akasema, “Ni mimi, Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”
Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”
26Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, “Chukueni mle; huu ni mwili wangu.” 27Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, “Kunyweni nyote katika kikombe hiki. 28Hii ni damu yangu ya agano ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi ili wasame hewe dhambi. 29Ninawahakikishia kuwa sitakunywa tena maji ya mzabibu mpaka siku nitakapoyanywa pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
Baba yangu.”
30Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa Mizeituni.
Yesu Amwambia Petro Atamkana
31Kisha Yesu akawaambia, “Usiku wa leo kila mmoja wenu atanikimbia kwa maana Maandiko yanasema, ‘Nitampiga mchungaji, na kondoo wote wa kundi lake watatawanyika.’ 32Lakini baada ya kufufuka, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
33Petro akasema, “Hata kama wote watakuacha, mimi sitaku acha.”
34Yesu akamjibu, “Ninakuambia kweli, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” 35Lakini Petro akasema, “Hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana.” Na wana funzi wote wakasema hivyo hivyo.
Gethsemane
36Kisha Yesu akaenda nao mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa, mimi ninakwenda mbele zaidi kuomba.” 37Akamchukua Petro, pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika na kuhuzunika. 38Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejaa majonzi karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, “Baba yangu, kama inawezekana, niondolee kikombe hiki cha mateso, lakini si kama nipendavyo bali kama upendavyo wewe.”
40Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwul iza Petro, “Hamkuweza kukesha nami hata kwa saa moja? 41Kesheni muombe, msije mkaingia katika majaribu. Kwa maana roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 42Akaenda tena mara ya pili, akaomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kion dolewe pasipo mimi kukinywea, mapenzi yako yafanyike.” 43Ali porudi tena aliwakuta wamelala kwa maana macho yao yalikuwa mazito. 44Kwa hiyo akawaacha akaenda tena mara ya tatu, akaomba vile vile.
45Kisha akarudi kwa wale wanafunzi akawaambia, “Bado mme lala na kupumzika? Angalieni, saa imefika ambapo mimi Mwana wa Adamu sina budi kukabidhiwa mikononi mwa wenye dhambi. 46Amkeni, twendeni! Yule anayenisaliti atafika sasa hivi!”
Yesu Akamatwa
47Alipokuwa anazungumza, Yuda, mmojawapo wa wale kumi na wawili, akafika,akifuatana na umati wa watu wenye mapanga na mar ungu. Walikuwa wametumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
48Yuda alikuwa amepatana na hao watu kuwa, ‘Nitakayembusu ndiye, mkamateni.’ 49Basi alipofika, alimwendea Yesu moja kwa moja, akamsalimia, “Salaam, Rabi!” Akambusu. 50Yesu akamjibu, “Rafiki, umekuja kufanya nini hapa?” Basi wale watu wakasogea, wakamkamata Yesu. 51Ndipo mmojawapo wa wafuasi wa Yesu ali poona hivyo, akachukua panga lake, akampiga nalo mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 52Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 53Unadhani siwezi kumwomba Baba yangu aniletee mara moja majeshi kumi na mbili ya malaika? 54Lakini nikifanya hivyo yatatimiaje Maandiko yale yasemayo kwamba mambo haya lazima yato kee?”
55Wakati huo Yesu akawaambia ule umati, “Mmekuja kunika mata kama mnyang’anyi kwa mapanga na marungu? Mbona siku zote nilikaa Hekaluni na kufundisha lakini hamkunikamata? 56Lakini haya yametokea ili Maandiko ya manabii yatiimie.” Ndipo wana funzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
Yesu Ashtakiwa Mbele Ya Baraza
57Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekutanika.
58Lakini Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu akaingia ndani pamoja na walinzi aone litakalotokea. 59Basi makuhani wakuu na baraza zima wakatafuta ushahidi wa uongo ili wamwue Yesu, 60lakini hawakupata, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza watu wawili, 61wakasema: “Huyu mtu alisema, ‘Nina uwezo wa kuvunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena katika muda wa siku tatu .’ ”
62Kisha kuhani mkuu akasimama, akamwambia Yesu, “Huna jibu? Husikii huo ushahidi waliotoa watu hao?” 63Lakini Yesu hakusema neno. Basi kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa jina la Mungu aliye hai, tuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.”
Mungu.”
64Yesu akajibu, “Umetamka mwenyewe. Lakini nina waambieni nyote kwamba baada ya hapa, mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa Mungu mwenye uweza na akija juu ya mawingu ya mbin guni.”
65Aliposikia maneno hayo, kuhani mkuu alirarua mavazi yake akasema, “Amekufuru! Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Si mmemsi kia akikufuru? 66Mnaamuaje?” Wakajibu, “Anastahili kufa!”
67Kisha wakamtemea mate usoni; wengine wakampiga ngumi na makofi, 68wakasema, “Hebu toa unabii wewe Kristo! Ni nani ame kupiga?”
69Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”
71Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 72Akakana tena kwa kiapo akisema, “Simfa hamu mtu huyo!” 73Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.