Yesu Amponya Mwenye Ukoma
1Alipotoka mlimani, umati mkubwa wa watu walimfuata. 2 Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” 3 Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake. 4 Na Yesu akamwambia, “Usiseme cho chote kwa mtu ye yote, lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe uthibitisho kwa watu kwamba umepona.”
Yesu Amponya Mtumishi Wa Askari
5 Yesu alipoingia Kapernaumu, askari mmoja alikuja kumwomba msaada, 6 akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani ame pooza, tena ana maumivu makali.” 7 Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.” 8 Lakini yule askari akamwambia, “Bwana, mimi sis tahili wewe uingie nyumbani kwangu; lakini sema neno tu, na mtumi shi wangu atapona. 9 Mimi niko chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Nikimwambia askari mmoja ‘Nenda 10 Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Nawaambia kweli, hata katika Israeli sijaona imani ya namna hii. 11 Ninawahakikishia kwamba wengi watatoka mashar iki na magharibi nao wataketi mezani pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni. 12 Lakini wana wa ufalme watatupwa nje gizani, huko watu watalia na kusaga meno.” 13 Yesu akamwambia yule askari, “Nenda nyumbani, na yale uliy oamini yatimie kwako.” Na yule mtumishi akapona tangu wakati ule ule.
Yesu Aponya Wengi
14 Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wake amelala akiwa ana homa. 15 Akamgusa mkono na homa ikam toka, akaamka akaanza kumhudumia. 16 Jioni ile walimletea watu wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno lake, na akawaponya wagonjwa wote. 17 Miujiza hii ilitimiza yale yali yosemwa na nabii Isaya kwamba: “Alichukua udhaifu wetu, na kubeba magonjwa yetu.”
18 Yesu alipoona umati wa watu unazidi kuongezeka aliwaamuru wanafunzi wake wavuke, waende ng’ambo ya pili. 19 Na mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu akamwambia, “Mwalimu, mimi nitaku fuata po pote utakapokwenda.” 20 Lakini Yesu akamjibu, “Mbweha wana mashimo yao, na ndege wa angani wana viota vyao, lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulaza kichwa changu.” 21 Mwana funzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” 22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, waache wal iokufa wawazike wafu wao.”
Yesu Atuliza Dhoruba
23 Alipoingia kwenye mashua wanafunzi wake walimfuata. 24 Mara dhoruba kali ikavuma na mawimbi yakakaribia kuzamisha ile mashua; lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakaenda kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunaangamia!”
26 Lakini Yesu akawajibu, “Enyi wenye imani haba, mbona mnaogopa?” Akasimama, akaikemea dhoruba na mawimbi; navyo vikat ulia, pakawa shwari kabisa. 27 Wanafunzi wake wakashangaa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu, ambaye hata upepo na bahari vinamtii?”
28 Walipofika ng’ambo ya Genezareti, watuwawili wenye pepo walikutana naye. Watu hawa waliishi makaburini na walikuwa wanat isha, kiasi kwamba hakuna mtu aliyethubutu kupita njia ile. 29 Wakapiga kelele, “Unataka nini kwetu, wewe Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kutimia?” 30 Mbali kidogo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Ukitufukuza, tafadhali turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.” 32 Akawaambia, “Nendeni”. Basi waka toka wakawaingia wale nguruwe; na kundi lote likatimka mbio kuelekea ukingoni mwa bahari, wakaangamia katika maji. 33 Wachungaji wa hao nguruwe wakakimbilia mjini wakaeleza kila kitu, na yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo. 34 Watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Wali pomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.