Mafarisayo Wadai Ishara
1Mafarisayo na Masadukayo walikuja kwa Yesu, wakiwa na nia ya kumtega. Kwa hiyo wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbin guni. 2 Akawajibu, “Ifikapo jioni mnasema, ‘Kwa kuwa anga ni nyekundu, hali ya hewa itakuwa nzuri.’ 3 Na asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na mvua kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yame tanda.’ Mnajua jinsi ya kusoma dalili za anga, lakini hamwezi kutambua dalili za nyakati. 4 Kizazi cha waovu na watu wasio waaminifu hutafuta ishara. Lakini hakitapewa ishara yo yote isi pokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.
Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo
5 Walipokwisha kuvuka hadi ng’ambo ya pili ya ziwa, wanafunzi wake waligundua kuwa walisahau kuchukua mikate. 6 Yesu akawaam bia, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.” 7 Wakabishana kati yao wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.”
8 Lakini Yesu, akitambua mazungumzo yao, alisema, “Enyi watu wenye imani haba! Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? 9 Bado tu hamwelewi? Hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu elfu tano na idadi ya vikapu vya mabaki mlivyokusanya? 10 Au ile mikate saba iliyolisha watu elfu nne na idadi ya vikapu vya mabaki mlivyokusanya? 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sizungumzii habari za mikate? Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hazungumzii juu ya hamira ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
Petro Amkiri Yesu Kuwa Ni Mwana Wa Mungu
13 Basi Yesu alipofika katika wilaya ya Kaisaria Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi Mwana wa Adamu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmo jawapo wa manabii.” 15 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
Mwana wa Mungu aliye hai.”
17 Na Yesu akamwambia, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni. 18 “Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda. 19 Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni na lo lo te utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
20 Kisha akawakataza wasimwambie mtu ye yote kwamba yeye ndiye Kristo.
Yesu Anazungumza Juu Ya Mateso Yake
21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.
22 Petro akamchukua kando akaanza kumkemea akamwambia, “Mungu apishie hayo mbali! Jambo hili halitakupata kamwe!” 23 Lakini Yesu akageuka akamwambia Petro , “Toka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo hayo si ya Mungu bali ya binadamu.”
24 Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu akitaka kuni fuata, ni lazima ajikane mwenyewe na achukue msalaba wake, anifu ate. 25 Kwa maana mtu akitaka kuokoa nafsi yake, ataipoteza; lakini mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataipata tena.
26 “Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini akaipoteza nafsi yake? Au mtu atabadilisha nini na nafsi yake? 27 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja katika utukufu wa Baba yangu pamoja na malaika wangu na nitamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 28 Nawaambieni kweli, baadhi yenu hapa hawataonja kifo kabla ya kuniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika Ufalme wangu.”