Yesu Abadilika Sura Mlimani
1Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, wakaenda peke yao juu ya mlima mrefu. 2 Na wakiwa huko, Yesu akabadilika sura mbele yao, uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama mwanga. 3 Na mara Musa na Eliya wakawatokea, wakawa wakizungumza na Yesu. 4 Kisha Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Ukiniruhusu, nitatengeneza vibanda vitatu hapa: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Eliya.”
5 Petro alipokuwa bado akizungumza, ghafla, wingu linalong’aa likatanda juu yao na sauti ikatoka kwenye wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye; msikilizeni yeye.” 6 Wanafunzi waliposikia haya walianguka chini kifudifudi wakajawa na hofu. 7 Lakini Yesu akaja, akawagusa, akawaambia, “Inukeni. Msiogope.” 8 Walipoinua macho yao hawakumwona mtu mwingine isipokuwa Yesu peke yake.
9 Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaambia, “Msimwambie mtu ye yote maono haya mpaka mimi Mwana wa Adamu nitakapofufuliwa kutoka kwa wafu.” 10 Wale wanafunzi wakamwuliza, “Kwa nini basi walimu wa sheria wanasema kwamba lazima Eliya aje kwanza?”
11 Akawajibu, “Ni kweli, Eliya lazima aje kwanza kurekeb isha mambo yote. 12 Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua, bali walimtendea walivyotaka. Na mimi Mwana wa Adamu pia watanitesa.” 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza kuhusu Yohana Mbatizaji.
Yesu Amponya Kijana Mwenye Kifafa
14 Alipofikia ulipokuwa umati wa watu, mtu mmoja alimjia Yesu akapiga magoti mbele yake akasema, 15 “Bwana, mwonee huruma mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara nyingi huan guka motoni na kwenye maji. 16 Nimemleta kwa wanafunzi wako laki ni hawakuweza kumponya.”
17 Yesu akajibu, “Ninyi kizazi kipotovu msioamini, nitakaa nanyi mpaka lini na nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa kwangu.” 18 Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu wakati huo. 19 Kisha wanafunzi wakam wendea Yesu kwa siri wakamwuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kum toa? ” 20 Akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Nina waambieni kweli, mkiwa na imani kama punje ndogo ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale’ nao utaondoka; na hakuna ambalo halitawezekana kwenu.” [ 21 “Lakini pepo wa aina hii hatoki ila kwa kuomba na kufunga.”]
22 Siku moja walipokuwa pamoja Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Adamu atawekwa mikononi mwa watu. 23 Nao watamwua na siku ya tatu atafufuka.” Wakasikitika sana.
Yesu Na Petro Watoa Kodi Ya Hekalu
24 Yesu na wanafunzi wake walipofika Kapernaumu, wakusanyaji kodi ya Hekalu walimjia Petro wakamwuliza, “Je, mwalimu wako hulipa kodi ya Hekalu?” 25 Petro akajibu, “Ndio, analipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kusema, akamwuli za, “Unaonaje Simoni’ wafalme wa ulimwengu hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Unadhani kutoka kwa jamaa zao au kutoka kwa wageni?” 26 Petro akamjibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akam wambia, “Kwa hiyo jamaa zao wamesamehewa. 27 Lakini ili tusi waudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemkamata; mfungue kinywa chake nawe utakuta fedha zinazo tosha kulipia kodi yangu na yako; ichukue ukawalipe.”