Yohana 18:28
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa wakampeleka kwenye ikulu ya gavana wa Kirumi. Ilikuwa ni alfa jiri. Wayahudi waliokuwa wanamshtaki Yesu hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa wachafu kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika sikukuu ya Pasaka.