Wakaribisheni Wenye Imani Dhaifu
1Kama mtu ana imani dhaifu mkaribisheni bila kubishana naye kuhusu maoni yake. 2 Imani ya mtu mmoja inaweza kumruhusu kula kila kitu, ambapo mwingine ambaye imani yake ni dhaifu anakula mboga za majani tu. 3 Mtu anayekula kila kitu asimhukumu yule asiyeweza kula kila kitu. Wala mtu ambaye hawezi kula kila kitu asimdharau yule anayekula kila kitu, kwa maana Mungu amemkubali. 4 Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Ni bwana wake tu awezaye kuamua kama amesimama au ameanguka. Naye atasi mama kwa sababu Bwana anaweza kumfanya asimame.
5 Mtu mmoja anahesabu siku fulani kuwa ni bora kuliko nyin gine na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. 6 Anayehesabu siku moja kuwa takatifu hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye anayekula nyama hufanya hivyo kwa kumtukuza Bwana, kwa maana humshukuru Mungu. Hali kadhalika akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa kum heshimu Bwana na humshukuru Mungu. 7 Kwa maana hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe na wala hakuna hata mmoja wetu anayekufa kwa ajili yake mwenyewe. 8 Kama tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana; na pia kama tukifa tunakufa kwa ajili ya Bwana. Kwa hiyo basi, kama tunaishi au kama tunakufa, sisi ni mali ya Bwana.
9 Maana kwa sababu hii, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi awe Bwana wa wote: waliokufa na walio hai.
10 Basi kwa nini unamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kumbuka kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11 Kwa kuwa imeandikwa:“Kama niishivyo, asema Bwana, Kila goti litapigwa mbele yangu, na kila ulimi uta mtukuza Mungu. 12 Kwa hiyo kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa
Usimkwaze Ndugu Yako
13 Basi, tuache kuhukumiana. Badala yake tuamue kuwa hatu tamkwaza ndugu kwa kitu cho chote. 14 Ninajua hakika kuwa nikiwa katika Bwana Yesu hakuna kitu cho chote ambacho kwa asili yake ni najisi. Lakini kwa mtu anayeamini kuwa kitu fulani ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15 Kama ndugu yako anahu zunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Usiruhusu kile ambacho unachokiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17 Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani na furaha ndani ya Roho Mtakatifu. 18 Kwa maana mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na anakubaliwa na wanadamu.
19 Kwa hiyo basi, tufanye kila juhudi tutimize yale yaletayo amani na kujengana. 20 Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Vyakula vyote vinafaa, lakini ni kosa kula kitu ambacho kinamfanya mwenzako kujikwaa. 21 Ni afadhali usile nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lo lote litakalomfanyandugu yako aanguke. 22 Unavyoamini kuhusu mambo haya, iwe ni siri yako na Mungu. Amebarikiwa mtu ambaye hajisikii kuhukumiwa afanyapo jambo analoamini kuwa ni sawa. 23 Lakini mtu mwenye mashaka kuhusu anachokula, amehukumiwa ikiwa atakula, kwa sababu kula kwake hakutokani na imani. Kwa maana jambo lo lote ambalo halito kani na imani, ni dhambi.