Warumi 15

1Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika imani. 3Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata mimi.” 4Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini. 5Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kuhusu Umoja

7Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea, ili Mungu apate kutukuzwa. 8Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9Na pia ili watu wa mataifa mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko: “Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba nyimbo za kulisifu jina lako.” 10Na tena yanasema, “Ninyi watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.” 11Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12Na tena Isaya anasema:“Shina la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote; na watu wa ma taifa watamtumaini.”

13Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.

Huduma Ya Paulo Kwa Mataifa

14Mimi nimeridhika ndugu zangu kuwa ninyi mmejaa wema, mnao ufahamu wote, tena mnaweza kujengana. 15Lakini kuhusu mambo fulani nimewaandikia kwa ujasiri nikiwa na shabaha ya kuwa kumbusha kwa sababu Mungu amenipa neema maalumu. 16Amenichagua kuwa mtumishi wa Kristo Yesu kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu, nitoe huduma ya kikuhani kwa kuitangaza Injili ya Mungu, ili watu wa mataifa wawe sadaka inayokubaliwa na Mungu na iliy otakaswa na Roho Mtakatifu.

17Kwa hiyo nina sababu ya kujisifu ndani ya Kristo kwa huduma yangu kwa Mungu. 18Hata sitasema juu ya jambo lo lote isipokuwa katika yale tu ambayo Kristo mwenyewe ameyafanikisha kwa kunitumia, katika maneno na matendo yangu, akawavuta watu wa mataifa wamtii akitumia 19nguvu za ishara na miujiza, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kuanzia Yerusalemu mpaka kando kando ya Iliriko nimekwisha kuhubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu. 20Shabaha yangu imekuwa nisihubiri mahali ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwin gine. 21Lakini kama ilivyoandikwa, “Wale ambao hawajaambiwa habari zake, wataona na wale ambao hawajasikia wataelewa.”

Paulo Apanga Kwenda Roma

22Hii ndio sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.

23Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimetamani sana kuja kwenu, 24natu maini kuwaona nikiwa safarini kwenda Spania, nifurahi kwa muda pamoja nanyi, kisha mnipatie msaada kwa safari hiyo. 25Ila sasa nakwenda kupeleka msaada kwa watu wa Mungu walioko Yerusalemu. 26Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yameamua kutoa mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu wasiojiweza walioko huko Yerusalemu. 27Wamependa kufanya hivyo lakini kwa kweli ni wajibu wao, maana kama watu wa mataifa mengine wameshiriki katika baraka za kiroho za Waisraeli, wanawajibika kuwahudumia Waisraeli katika mahitaji yao ya kimwili. 28Kwa hiyo baada ya kukamilisha kazi hii na kuhakikisha kuwa wamepokea kila kitu kilichokusanywa, nitakwenda Spania kupitia kwenu. 29Ninafahamu kwamba nitakapokuja kwenu, nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.

30Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, muwe pamoja nami mkiniombea kwa Mungu. 31Ombeni niepushwe na wale wasioamini walioko Uyahudi, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa na watu wa Mungu; 32ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, niburudishwe pamoja nanyi. 33Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.