Warumi 10

Kutokuamini Kwa Waisraeli

1Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwamba Waisraeli waokolewe. Ninashuhudia wazi kwamba wao wanajuhudi kubwa ya kumtumikia Mungu, lakini juhudi yao haitokani na kuelewa. Wameshindwa kuelewa haki itokayo kwa Mu ngu, na badala yake wakajaribu kujiwekea ya kwao; kwa hiyo hawa kutii haki ya Mungu. Kwa maana Kristo amekamilisha sheria ili kila mtu mwenye imani ahesabiwe haki.

Wokovu Ni Kwa Wote

Musa anaandika kwamba mtu anayejaribu kutenda haki kwa msingi wa sheria ataishi kwa sheria. Lakini haki itokanayo na imani husema hivi, “Usiseme nafsini mwako, ‘Ni nani atapaa mbi nguni?”’ yaani kumleta Kristo duniani, au “‘Ni nani atashuka kuzimuni?”’yaani kumleta Kristo kutoka kwa wafu. Bali inasema hivi, “Neno la Mungu liko karibu nawe; liko mdomoni mwako na moyoni mwako,” yaani, neno la imani tunayohubiri. Kama ukikiri kwa kinywa chako kuwa Yesu ni Bwana na ukiamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10 Kwa maana mtu ana poamini moyoni mwake huhesabiwa haki, na anapokiri kwa kinywa chake, huokolewa. 11 Kama yasemavyo Maandiko, “Hakuna amwami niye ambaye ataaibika.” 12 Kwa maana hakuna tofauti kati ya wote naye huwabariki wote wamwitao. 13 Kwa maana, “Kila mtu atakayeliita Jina la Bwana, ataokoka.”

14 Lakini watu watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Na watamwaminije yeye ambaye hawajawahi kumsikia? Na watamsikiaje kama mtu hakuwahubiria? 15 Na watu watahubirije kama hawaku tumwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri mno miguu ya hao wanaohubiri Habari Njema!”

16 Lakini si wote walioipokea Habari Njema. Kwa maana Isaya alisema:“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17 Basi, chanzo cha imani ni kusikia, na kusikia huja kwa kuhubiri neno la Kristo. 18 Lakini nauliza, hivi wao hawajasikia? Hakika wame sikia; kwa maana Maandiko yanasema: “Sauti yao imeenea duniani kote, na maneno yao yamefika miisho ya ulimwengu.” 19 Nauliza tena, je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza Musa anasema, “Nitawa fanya muone wivu kwa ajili ya wale ambao hawajawa taifa bado; nitawafanya mkasirike kwa ajili ya taifa la watu wasio elewa.” 20 Na Isaya anasema kwa ujasiri, “Wale ambao wali kuwa hawanitafuti, wamenipata. Nimejidhihirisha kwa wale ambao walikuwa hawaniulizii.” 21 Lakini kuhusu wana wa Israeli anasema: “Mchana kutwa nimewanyooshea mikono watu wakaidi na wasiotii.”